KUMBARIKI MGONJWA

Generic placeholder image
Kumbariki Mgonjwa:

Padri anapowatazama wagonjwa hospitalini au nyumbani bila kuwapa Sakramenti, aweza kusema hivi:
P. Tumsifu Yesu Kristo.
W. Milele. Amina.

KWA MTU MZIMA
P. Bwana Yesu Kristo awe nawe ili akulinde.
W. Amina
P. Awe mbele yako ili akuongoze, awe nyuma yako ili akuimarishe.
W. Amina
P. Akutazame, akutunze na akubariki
W. Amina
P. Yeye anayeishi na kutawala pamoja na Baba na Roho Mtakatifu milele.
W. Amina.

P. Baraka ya Mungu Mwenyezi, ya Baba + na ya Mwana naya Roho Mtakatifu ikushukie na kukaa kwako daima.
W. Amina

KWA WATOTO
Tuombe. Ee Mungu, umewapangia malaika na wanadamu kazi zao kwa azimio la ajabu. Basi ukubali kwa wema wako, wale wanaosimama daima mbele yako mbinguni wakutumikie, wayalinde maisha ya mtoto huyu hapa duniani. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
W. Amina.

P. Baraka ya Mungu Mwenyezi, ya Baba + na ya Mwana na ya Roho Mtakatifu ikushukie na kukaa kwako daima.
W. Amina.