Des 26 Mt. Stefano Shahidi
MASOMO
SOMO 1: Mdo.6:8-10,7:54-60
Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya
watu wa sinagogi lilioitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia
na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho
aliyesema naye. Basi waliposikia maneno yake wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho
Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona, utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa
mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama, naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa
kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje
ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga
kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu,
Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.31:2-3,5-7,16,20
1. Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
Ndiwe genge langu na ngome yangu;
Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. (K)
(K) Mikononi mwako, naiweka roho yangu, Ee Bwana.
2. Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.
Bali mimi namtumaini Bwana.
Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako. (K)
3. Umwangaze mtumishi wako
Kwa nuru ya uso wako;
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. (K)
Shangilio
Aleluya, aleluya,
Abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana; Bwana ndiye aliyetupa nuru.
Aleluya.
INJILI: Mt.10:17-22
na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu,
kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema;
maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani
yenu. Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao,
na kuwafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia
hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
MAOMBI
Ee Mungu, leo tunapofanya Sikukuu ya Mt. Stefano, Shemasi na Shahidi wako wa kwanza, twakuomba:
Kiitikio: Kwa huruma yako utusikie.
1. Uwajalie Baba Mtakatifu wetu F., maaskofu, mapadre na mashemasi wetu wote ujasiri wa
kushikilia bila woga imani, itikadi sahihi, mapokeo na mfundisho yote ya Kanisa lako.
2. Waamini wako wote wadumu katika imani waliyokiri siku ya Ubatizo na kuitangaza kwa maneno na matendo mema,
hata wakati wa mateso.
3. Utuamshie moyo ule aliokuwa nao Mt. Stefano, tupate kuwaombea hata maadui zetu, kuzikabidhi roho zetu
kwako na kupata kifo chema.
4. Uwaepushe na kishawishi cha usaliti wote wenye matatizo ya kiroho na kimwili na uzipokee roho za marehemu
wetu huko mbinguni.
Ee Bwana, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na hila za adui yetu shetani; tupate kukutumikia kiaminifu mpaka
kufa kama alivyofanya Mt. Stefano. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.