Neno letu kwako

Utangulizi

Kwanza tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuikamilisha kazi hii. Pia tunapenda kuwashukuru kundi la Umoja wa Vijana Jimbo katoliki Tanga Tanzania, waliochochea utengenezaji wa kazi hii. lengo kubwa ni kuwawezesha vijana wanapokutana waweze kusali sala zetu za kanisa kwa njia rahisi kwa kutumia tu simu zao za mkononi.

Pomoja na hilo kazi hii itakuwa pia masaada mkubwa kwa Maklero na hata watawa wetu ambao muda wote husali sala hizi za kanisa hata wawapo safarini. Kumbe uwepo wa sala hizi katika simu zao pia kutawezesha kufikia lengo la kusali bila hata kuwa na kitabu cha sala. Tuitumia Teknolojia iliyopo katika kutimiza shughuli zetu tukimtukuza Mungu popote pale tulipo.

Kazi hii imeweka masomo ya kila siku, Jumapili na baadhi ya sikukuu za kanisa katoliki kulingana na Shajara ya kanisa mahalia la Tanzania kufuatana na muongozo wa baraza la maaskofu TEC. Pia humo kuna sala mbalimbali zinazotumiwa na waamini mara kwa mara katika kumtukuza Mungu, kama sala ya Rozari na hata njia ya Msalaba. Pia kazi hii imeweka Biblia Takatifu inayotumiwa na wakatoliki, yaani Biblia yenye vitabu vya Deoterokanoni. Pia kuna maadhimisho ya sakarament mbalimbali katika kanisa. Mungu ni mwema kila wakati tumtukuze kwa sala na matendo yetu. Amina

  • Pd. Richard Jelas Kimbwi
    Kanisa Katoliki Tanga, Tanzania.