ANGELUS

MALAIKA WA BWANA
Husaliwa kipindi chote cha mwaka isipokua wakati wa Pasaka

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
- Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Ndimi mtumishi wa Bwana.
- Nitendewe ulivyonena.

Salamu, Maria...

Neno wa Mungu akatwaa mwili.
- Akakaa kwetu.

Salamu, Maria...

Utuombee Mzazi mtakatifu wa Mungu.
- Tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe

Tunakuomba, ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika kwamba Mwanao amejifanya mtu, kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.


MALKIA WA MBINGU
Husaliwa kipindi cha Pasaka.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Malkia wa mbingu furahi, Aleluya,
- Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka alivyosema, Aleluya.
- Utuombee kwa Mungu Aleluya.
Furahi, shangilia, ee Bikira Maria, Aleluya.
- Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya.

Tuombe.

Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo, Mwanao: fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, Mamaye, tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.