SALA YA CHAKULA NA SALA YA KAZI

KABLA YA KULA
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Utubariki, Mungu wetu, sisi na chakula chetu, tupate nguvu za kukutumikia vema. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

KISHA KULA
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Twakushukuru Mungu wetu, kwa chakula ulichotupatia, tumepata nguvu za kukutumikia vema. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

KABLA YA KAZI
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Uje Roho Mtakatifu uzienee nyoyo za waamini wako, uwatie mapendo yako. Peleka Roho wako, vitaumbwa upya. Na nchi itageuka.

Tuombe

Ee Mungu, uliyefundisha nyoyo za waamini ukiwaletea mwanga wa Roho Mtakatifu, tunaomba tuongozwe na yule Roho, tupende yaliyo mema tupate daima faraja zake. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo, Bwana wetu. Amina.

Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

KISHA KAZI
Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

Tunakimbilia ulinzi wako, Mzazi mtakatifu wa Mungu; usitunyime tukiomba katika shida zetu; utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, ewe Bikira mtukufu uliyebarikiwa. Amina.

Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.