ROZARI TAKATIFU JUMATATU
MATENDO YA FURAHA

Generic placeholder image

1: Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu: Amina.

2: Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wambingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.

3: Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.

4.-: Naye atuzidishie imani.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

-: Naye atuongezee matumaini.
Salamu Maria...

-: Naye atuwashie mapendo.
Salamu Maria...

Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina

5: Matendo ya furaha
5.1: Tendo la kwanza: Malaika anampasha habari Maria kwamba atakuwa Mama wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Baba yetu...
Salamu Maria... (mara kumi)
Atukuzwe Baba...
Ee Yesu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho za watu wote mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako kuliko wengine.

5.2: Tendo la pili: Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti.
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Baba yetu...
Salamu Maria... (mara kumi)
Atukuzwe Baba...
Ee Yesu...

5.3: Tendo la tatu: Yesu anazaliwa Bethlehemu.
Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
Baba yetu...
Salamu Maria... (mara kumi)
Atukuzwe Baba...
Ee Yesu...

5.4: Tendo la nne: Yesu anatolewa hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Baba yetu...
Salamu Maria... (mara kumi)
Atukuzwe Baba...
Ee Yesu...

5.5: Tendo la tano: Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa zetu.
Baba yetu...
Salamu Maria... (mara kumi)
Atukuzwe Baba...
Ee Yesu...

SALAMU MALKIA:
Salamu, Malkia, Mama mwenye huruma; uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi, mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni huu, utuoneshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu, Bikira Maria.

K. Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:
Ee Mungu, makimbilio na nguvu yetu, uwaangalie kwa wema watu wanaokulilia; na kwa maombezi ya Bikira Maria mtukufu asiye na kosa, Mzazi wa Mungu, na ya Mtakatifu Yosefu, mume wake, na ya watakatifu Petro na Paulo mitume wako, na ya watakatifu wote: usikilize kwa huruma na wema sala tunazokutolea kwa wongofu wa wakosefu na kwa uhuru na utukufu wa Kanisa, Mama mtakatifu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

6: LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie = Bwana ut...
Kristo utuhurumie = Kristo ut...
Bwana utuhurumie = Bwana ut...
Kristo utusikie = Kristo utusikilize
Baba wa mbinguni, Mungu, = utuhurumie.
Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu, = utuh...
Roho Mtakatifu, Mungu, = utuh...
Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, = utuh...
Maria Mtakatifu, = utuombee...
Mzazi Mtakatifu wa Mungu, = utuo...
Bikira Mtakatifu, mkuu wa mabikira, = ut...
Mama wa Kristo, = ut...
Mama wa Kanisa, = ut...
Mama wa huruma, = ut...
Mama wa neema ya Mungu, = ut...
Mama wa matumaini = ut...
Mama Mtakatifu sana, = ut...
Mama mwenye usafi wa moyo, = ut...
Mama usiye na doa = ut...
Mama usiye na dhambi, = ut...
Mama mpendelevu, = ut...
Mama mstaajabivu = ut...
Mama wa shauri jema, = ut...
Mama wa Muumba = ut...
Mama wa Mkombozi, = ut...
Bikira mwenye utaratibu, = ut...
Bikira mwenye heshima, = ut...
Bikira mwenye sifa, = ut...
Bikira mwenye enzi, = ut...
Bikira mwenye huruma, = ut...
Bikira amini, = ut...
Kioo cha haki, = ut...
Kikao cha hekima, = ut...
Sababu ya furaha yetu, = ut...
Chombo cha neema, = ut...
Chombo cha heshima, = ut...
Chombo bora cha ibada, = ut...
Waridi lenye fumbo, = ut...
Mnara wa Daudi, = ut...
Mnara wa pembe, = ut...
Nyumba ya dhahabu, = ut...
Sanduku la agano, = ut...
Mlango wa mbingu, = ut...
Nyota ya asubuhi, = ut...
Afya ya wagonjwa, = ut...
Makimbilio ya wakosefu, = ut...
Mfariji wa wahamiaji = ut...
Mfariji wa wenye uchungu, = ut...
Msaada wa wakristo, = ut...
Malkia wa Malaika, = ut...
Malkia wa Mababu, = ut...
Malkia wa Manabii = ut...
Malkia wa Mitume, = ut...
Malkia wa Mashahidi = ut...
Malkia wa Waungama, = ut...
Malkia wa Mabikira, = ut...
Malkia wa Watakatifu wote, = ut...
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili, = ut...
Malkia uliyepalizwa mbinguni, = ut...
Malkia wa Rozari takatifu, = ut...
Malkia wa familia, = ut...
Malkia wa amani, = ut...
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za ulimwengu = utuhurumie. (mara tatu)

K. Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Ee Bwana Mungu, twakuomba utujalie sisi watumishi wako tuwe siku zote na afya ya roho na mwili; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakatifu, Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya sasa, tupate na furaha za milele. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

Kumbuka:
Kumbuka, ee Bikira Maria mwenye rehema, haijasikika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi Wako, akiomba shime kwako, akitaka umwombee. Nami kwa matumaini hayo, nakukimbilia, ee Mama, mkuu wa mabikira; ninakuja kwako, nasimama mbele yako mimi mkosefu, ewe Mama wa Neno wa Mungu, usiyakatae maneno yangu, bali uyasikilize kwa wema, na unitimizie. Amina.

Kwa jina la Baba la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina