UTARATIBU WA MAISHA YA WAKRISTO

- Asubuhi ninapoamka, nafanya ishara ya Msalaba nikisali sala ya asubuhi.
- Naweka nia njema kwa kazi na matendo mema. Nikipata nafasi nashiriki Misa takatifu pia siku za kazi.
- Mchana nafanyakazi kwa juhudi, nipate mahitaji duniani na tuzo mbinguni.
- Kabla ya kula naomba baraka na baada ya kula nashukuru.
- Jioni kabla ya kulala nasali na kufanya sikitiko timilifu; kisha hujinyunyizia maji ya baraka kujibariki kwa ishara ya msalaba.
- Kila Dominika, Sherehe na Sikukuu na iadhimisha kitakatifu kama nilivyoamriwa.
- Napokea Sakramenti mara nyingi, nipate nguvu na ukamilifu.
- Ijumaa Kuu nayakumbuka mateso ya Yesu, nikijikatalia nyama kwa ajili yake.
- Napendana na wenzangu. Nawaheshimu wakubwa wangu, nawasaidia wenye shida. Nawaangalia wagonjwa.
- Nikipatwa na vishawishi nakataa mara na kusali. Naepuka nafasi za dhambi kama watu wabaya na mashauri mabaya.
- Nikishikwa na ugonjwa au taabu, navumilia pamoja na Yesu, nipate kutubu na kuongeza stahili zangu.

Matendo ya Huruma
(Papa Fransisko, Misericordiae-vultus, 11 Aprili 2015)"
Hebu tuyagundue upya haya matendo ya huruma ya kimwili:
1. Kulisha wenye njaa.
2. Kuwanywesha wenye kiu.
3. Kuwavika walio uchi.
4. Kuwakaribisha wageni.
5. Kuwaponya wagonjwa.
6. Kuwatembelea wafungwa.
7. Kuzika wafu.

Na tusiyasahau matendo ya huruma ya kiroho:
1. Kuwashauri walio mashakani.
2. Kuwafunza wajinga.
3. Kuwaonya wadhambi.
4. Kuwafariji waliojeruhiwa.
5. Kusamehe maovu.
6. Kuchukuliana kwa saburi na wale wanaotutendea maovu.
7. Kuwaombea walio hai na wafu."