Generic placeholder image

ADHIMISHO LA MISA

Sala na Masomo angalia link ya masomo.

KANUNI YA MISA

Vifupisho:
K = Padre au Askofu
W = Waamini
KK= Kiongozi peke yake;
K1, K2, K3,... = Kuhani wa 1, wa 2, au 3,... peke yake
KW= Kiongozi na Makuhani wengine pamoja.

----------------
---------------

A. LITURUJIA YA NENO

Waamini wakisha kusanyika, kuhani anakwenda altareni pamoja na wahudumu, wakati huo wimbo wa kuingia huimbwa Anapofika altareni, anainama sana pamoja na wahudumu (au anapiga goti kuelekea tabernakulo, kama ipo), na anatoa heshima kwa altare kwa kuibusu. Wakati kuhani, akiwaelekea waamini, anasema:

K. Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
W. Amina.

kuhani anawasalimu watu
K. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote.
W. Na viwe rohoni mwako.

Au:
K. Neema na amani kutoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo, viwe nanyi.
W. Na viwe rohoni mwako.

Au.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.

Askofu. Amani iwe kwenu.
W. Na iwe rohoni mwako.

TOBA
K. Ndugu zangu, tukiri dhambi zetu, ili tupate kustahilishwa kuadhimisha mafumbo matakatifu.

Wote: Namwungamia Mungu mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo, na kwa kutotimiza wajibu: nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana namwomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi, ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.

Au:
K. Ee Bwana, utuhurumie.
W. Kwa kuwa tumekukosea.
K. Ee Bwana, utuoneshe huruma yako.
W. Utupe na wokovu wako.

Au:
K. Wewe uliyetumwa kuwaponya wanaotubu moyoni, Bwana, utuhurumie. (Kyrie, eleison.)
W. Bwana, utuhurumie. (Kyrie, eleison.)
K. Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu, Kristo, utuhurumie. (Christe, eleison.)
W. Kristo, utuhurumie. (Christe, eleison.)
K. Wewe uliyeketi kuume kwa Mungu Baba, ukituombea, Bwana, utuhurumie. (Kyrie, eleison.)
W. Bwana, utuhurumie. (Kyrie, eleison.)

K. Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele.
W. Amina.

-------------
BWANA UTUHURUMIE:
K. Bwana, utuhurumie.
W. Bwana, utuhurumie.
K. Kristo, utuhurumie.
W. Kristo, utuhurumie.
K. Bwana, utuhurumie.
W. Bwana, utuhurumie.

Au:
K. Kyrie, eleison.
W. Kyrie, eleison.
K. Christe, eleison.
W. Christe, eleison.
K. Kyrie, eleison.
W. Kyrie, eleison.

UTUKUFU (GLORIA)
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
na amani duniani kwa watu aliowaridhia.
Tunakusifu, tunakuheshimu,
tunakuabudu, tunakutukuza,
tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu,
ee Bwana Mungu, Mfalme wa mbinguni,
Mungu Baba mwenyezi.
Ee Bwana Yesu Kristo, Mwana pekee,
ee Bwana Mungu, Mwanakondoo wa Mungu, Mwana wa Baba,
mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu, utuhurumie;
mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu, pokea ombi letu.
Mwenye kuketi kuume kwa Baba, uhurumie.
Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako Mtakatifu,
peke yako Bwana, peke yako Uliye juu kabisa, Yesu Kristo,
pamoja na Roho Mtakatifu,
katika utukufu wa Mungu Baba. Amina.

TUOMBE:
SALA/KOLEKTA
kolekta na masomo yote tazama link ya masomo hapo chini.
Baada ya masomo na mahubiri hufuata kanuni ya imani pale inapoagizwa kusaliwa.

KANUNI YA IMANI
Kanuni ya imani ya Nikea-Kostantinopoli
Nasadiki kwa Mungu mmoja, Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli, aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba, ambaye vitu vvote vimeumbwa naye. Alishuka kutoka mbinguni, kwa ajili yetu sisi wanadamu, na kwa ajili ya wokovu wetu. Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu. Akasulubiwa kwa ajili yetu sisi, kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato; akateswa, akafa na akazikwa. Siku ya tatu akafufuka, kadiri ya Maandiko, akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Baba. Atakuja tena kwa utukufu, kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana na mleta uzima, atokaye kwa Baba na Mwana. Anayeabudiwa na kutukuzwa, pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii. Nasadiki kwa Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume. Naungama Ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi. Nangojea na ufufuko wa wafu, na uzima wa milele ijayo. Amina.

KANUNI YA IMANI
Kanuni ya imani ya Mitume. Kanuni ya imani ya Ubatizo ya Kanisa la Roma.
Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na dunia, na kwa Yesu Kristo, Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu. Siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.

SALA ZA WAAMINI
K. Ndugu zangu, tumwombe Mungu Baba mwenyezi asikilize kwa wema sala zetu kwa ujumbe wa Yesu Kristo, Bwana wetu.

Kisha hufuata maombi yaliyoandaliwa.

K. Ee Mungu uliye makimbilio na nguvu yetu, uliye asili ya wema wote, usikilize sala za Kanisa lako, utujalie ili hayo tunayoomba kwa imani tuyapate kweli. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
W. Amina.

B. LITURUJIA YA EKARISTI

Maandalizi ya mkate na divai:
Mkate:

K. Utukuzwe, ee Bwana, Mungu wa ulimwengu, maana kwa ukarimu wako tumepokea mkate huu tunaokutolea; ni mazao ya nchi na ya kazi ya mikono ya wanadamu, na uwe kwetu mkate wa uzima.
W. Atukuzwe Mungu milele.

K. akichanganya divai na maji:
kwa fumbo la maji haya na divai hii tujaliwe kushirikishwa umungu wake Yeye, aliyekubali kushiriki ubinadamu wetu.

Divai
K. Utukuzwe, ee Bwana, Mungu wa ulimwengu, maana kwa ukarimu wako tumepokea divai hii tunayokutolea; ni tunda la mzabibu na la kazi ya mikono ya wanadamu, na iwe kwetu kinywaji cha kiroho.
W. Atukuzwe Mungu milele.

K. kwa sauti ndogo.
Tukiwa na moyo wa unyenyekevu na toba tupokewe nawe, ee Bwana; na hivyo sadaka yetu ifanyike leo mbele yako, ili ipate kukupendeza, ee Bwana Mungu.

K. akinawa mikono.
Ee Bwana, unioshe kabisa uovu wangu, unitakase dhambi zangu.

K. Salini, ndugu, ili sadaka yangu na yenu ikubalike kwa Mungu Baba mwenyezi.
W. Bwana apokee sadaka mikononi mwako kwa sifa na utukufu wa jina lake, na kwa manufaa yetu sisi na ya Kanisa lake lote takatifu.

SALA YA KUOMBEA DHABIHU:
Tazama link ya masomo hapo chini

SALA YA EKARISTI

UTANGULIZI.

----------------
----------------

1. UTANGULIZI WA MAJILIO:
MAJILIO I:
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye, katika ujio wake wa kwanza, alipokuja katika unyenyekevu wa mwili, aliutimiza mpango ulioandaliwa nawe tangu kale. Hivyo, akatufungulia njia ya wokovu wa milele, ili, atakapokuja tena katika utukufu wa enzi yake, hatimaye tupewe waziwazi mema yaliyoahidiwa, ambayo kwa sasa tunathubutu kuyatarajia, tukikesha.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

MAJILIO II:
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye ambaye alitabiriwa na maaguzi ya manabii wote, Mama Bikira alimchukua kwa upendo wa ajabu, na Yohane Mbatizaji alishangilia kuja kwake na kumtambulisha alipofika. Yeye aliyetujalia kungojea kwa furaha fumbo la kuzaliwa kwake, atukute tukikesha katika sala na tukimshangilia kwa nyimbo za kumsifu.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

2. UTANGULIZI KUZALIWA BWANA:
KUZALIWA KWA BWANA I: Kristo ni mwanga.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Maana, kwa fumbo la Neno aliyetwaa mwili, mwanga mpya wa utukufu wako umetuangazia macho ya akili zetu; ili, tunapomjua Mungu katika hali ya kuonekana, kwa njia yake tuvutwe kuyapenda mambo yasiyoonekana.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KUZALIWA KWA BWANA II: Kufanywa yote upya katika Umwilisho wa Bwana.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Katika sikukuu ya fumbo hili takatifu, Yeye, ambaye kwa asili haonekani, ameonekana katika hali yetu ya kibinadamu. Naye aliyezaliwa tangu milele, wakati huu ameanza kuwepo kimwili, ili, kwa kuyainua ndani yake yote yaliyoanguka, autengeneze tena ulimwengu wote, na kumrudisha katika Ufalme wa mbinguni mwanadamu aliyepotea.
Kwa hiyo, nasi pamoja na Malaika wote tunakusifu, tukiimba kwa shangwe na furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KUZALIWA KWA BWANA III: Ubadilishano katika. Umwilisho wa Neno.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa njia yake leo umeangaza ubadilishano uliotufanya wapya, kwani, maadamu udhaifu wetu ulichukuliwa na Neno wako, si tu hali ya kibinadamu yenye kufa imebadilika na kupata heshima ya daima, lakini sisi pia, kutokana na ushirika huo wa ajabu naye, alitufanya kuwa wa milele.
Kwa hiyo, pamoja na Malaika wa mbinguni, tunakusifu tukiungama kwa furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

EPIFANIA YA BWANA: Kristo mwanga wa mataifa.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Maana, leo, Wewe mwenyewe umefunua fumbo la wokovu wetu katika Kristo kuwa mwanga wa mataifa. Alipotokea katika hali yetu yenye kufa, Wewe ulitutengeneza katika hali mpya ya utukufu wake wa milele.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

3. UTANGULIZI KWARESMA:
KWARESIMA I: Maana ya kiroho ya Kwaresima.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Maana, unawajalia kwa wema waamini wako wangojee kila mwaka kwa furaha mafumbo ya Pasaka, hali wametakaswa mioyo. Maadamu wanawajibika kwa bidii katika mazoezi ya ibada na matendo ya upendo, wakishiriki mara kwa mara mafumbo ya wokovu, ambayo kwayo walizaliwa upya, waongozwe kwenye utimilifu wa neema ya wana.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KWARESIMA II: Toba ya kiroho.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe uliwawekea vyema wanao kipindi maalumu kwa ajili ya kutakasa roho zao; ili wao, kwa kuyahamisha mawazo mbali na tamaa mbaya, waache kuyaegamia mambo yapitayo bali waambatane zaidi na yaliyo ya milele.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Watakatifu na Malaika wote, tunakusifu, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KWARESIMA III: Matunda ya kujinyima.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe ulitaka sisi tukutolee shukrani kwa kujinyima, ili kwa njia hiyo hata sisi wakosefu tuondolewe ukaidi, na, kwa kuwapatia chakula wahitaji, tufanywe waigaji wa ukarimu wako.
Kwa hiyo, Sisi pamoja na umati wa Malaika, tunakutukuza kwa sauti ya kukusifu, tukisema:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KWARESIMA IV: Matunda ya kufunga.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe, kwa njia ya mfungo wa kimwili unazuia vilema vyetu, unainua roho zetu, unatujalia fadhila na thawabu, kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Kwa njia yake Malaika husifu adhama yako, Enzio hukuabudu, na Mamlaka hukupigia magoti wakitetemeka. Mbingu na Nguvu za mbinguni, na Maserafi wenye heri, wakuadhimisha pamoja kwa shangwe.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukisema kwa sauti ya unyenyekevu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

MATESO YA BWANA I: Nguvu ya Msalaba.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa njia ya Mateso ya Mwanao yaletayo wokovu ulimwengu wote umejifunza kukiri adhama yako, wakati nguvu ya ajabu ya msalaba hudhihirisha hukumu ya ulimwengu na mamlaka ya Msulibiwa.
Kwa hiyo, ee Bwana, sisi nasi pamoja na Malaika na watakatifu wote, tunakusifu, tukisema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

MATESO YA BWANA II: Ushindi wa Mateso.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Tunatambua kwamba zimekaribia siku za mateso yake yaletayo wokovu na za ufufuko wake mtukufu, ambapo kiburi cha adui wa kale hushindwa, na fumbo la ukombozi wetu hufanywa upya. Kwa njia yake majeshi ya Malaika husujudia adhama yako, wakifurahi daima na milele mbele ya uso wako.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukishiriki kusema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

4. UTANGULIZI PASAKA
PASAKA I: Fumbo la Pasaka.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukutukuza kila wakati, ee Bwana, lakini hasa usiku huu (siku hii) ( wakati huu) kutangaza utukufu wako, kwa kuwa Kristo, Pasaka wetu, ametolewa sadaka.
Yeye ndiye Mwanakondoo wa kweli aliyeondoa dhambi za ulimwengu. Yeye ndiye aliyeangamiza mauti yetu kwa kufa kwake, na alitengeneza upya uzima kwa kufufuka kwake.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

PASAKA II: Maisha mapya katika Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukutukuza kila wakati, ee Bwana, lakini hasa wakati huu kutangaza utukufu wako, kwa kuwa Kristo, Pasaka wetu, ametolewa sadaka.
Kwa njia yake watoto wa nuru wanazaliwa katika uzima wa milele, na waamini wanafunguliwa makao ya ufalme wa mbinguni. Kwa kufa kwake tumekombolewa katika kufa kwetu, na katika ufufuko wake uzima wa wote umefufuliwa.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

PASAKA III: Kristo yu hai naye hutuombea daima.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukutukuza kila wakati, ee Bwana, lakini hasa wakati huu kutangaza utukufu wako, kwa kuwa Kristo, Pasaka wetu, ametolewa sadaka.
Yeye anaendelea kujitoa kwa ajili yetu, tena anatutetea siku zote mbele zako kama mwombezi; ndiye aliyetolewa sadaka wala hafi tena, bali yu hai daima, yeye aliyeuawa.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

PASAKA IV: Kutengenezwa upya ulimwengu kwa njia ya fumbo la Pasaka.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukutukuza kila wakati, ee Bwana, lakini hasa wakati huu kutangaza utukufu wako, kwa kuwa Kristo, Pasaka wetu, ametolewa sadaka.
Kwa maana, kwa kuyaharibu yale ya zamani, yote yaliyokuwa yameanguka yalifanywa upya, nasi tukarudishiwa ukamilifu wa uzima katika Kristo.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako. wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

PASAKA V: Kristo kuhani na kafara.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukutukuza kila wakati, ee Bwana, lakini hasa wakati huu kutangaza utukufu wako, kwa kuwa Kristo, Pasaka wetu, ametolewa sadaka.
Yeye, kwa sadaka ya mwili wake, alikamilisha kafara za zamani katika ukweli wa msalaba, na, kwa kujikabidhi kwako kwa ajili ya wokovu wetu, alijidhihirisha kuwa kuhani, altare na mwanakondoo.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KUPAA BWANA I: Fumbo la Kupaa kwake Bwana.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa maana Bwana Yesu, Mfalme wa utukufu, mshindi wa dhambi na mauti, amepaa (leo) juu mbinguni, huku Malaika wakimstaajabia. Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu, Hakimu wa ulimwengu na Bwana wa majeshi; amepaa siyo kwa kusudi la kuachana na unyonge wetu, bali, ili sisi, tulio viungo vyake, tukae tukiamini kwamba tutamfuata huko alikotutangulia Yeye aliye kichwa chetu na asili yetu.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KUPAA BWANA II: Fumbo la Kupaa kwake Bwana.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye baada ya kufufuka kwake alijidhihirisha wazi kwa wanafunzi wake wote, akapaa mbinguni mbele ya macho yao, ili atujalie sisi tuwe washiriki wa umungu wake.
Kwa sababu hiyo, katika upeo wa furaha ya kipasaka, ulimwengu mzima unashangilia. Lakini pia nguvu za mbinguni na majeshi ya Malaika wanaimba utenzi wa utukufu wako, wakisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

5. UTANGULIZI DOMINIKA ZA MWAKA
DOMINIKA “ZA MWAKA” I: Fumbo la Pasaka na taifa la Mungu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kazi yake aliyoifanya kwa njia ya fumbo la Pasaka ilikuwa ya ajabu, ili tupate kuitwa kutoka katika dhambi na nira ya mauti na kupewa utukufu huu wa kuitwa uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu. Wewe umetuita kutoka gizani na kutuingiza kwenye muru yako ya ajabu, tupate kutangaza popote maweza yako.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA “ZA MWAKA” II: Fumbo la wokovu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye, kwa kuwahurumia wanadamu makosa yao, alikubali kuzaliwa na Bikira. Yeye, akiisha kuteswa msalabani, alituokoa na mauti isiyo na mwisho, na, kwa kufufuka katika wafu, alitujalia uzima wa milele.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA "ZA MWAKA” III: Wokovu wa mwanadamu kwa njia ya mwanadamu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Sisi tunatambua kuwa ni fahari ya utukufu wako mkuu kuwasaidia kwa umungu wako wanadamu wenye hali ya kufa; lakini pia kutupatia dawa ya kutuponya tusidhurike na kufa kwenyewe; na kuwaokoa waliopotea kutoka kule walikopotelea kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa njia yake majeshi ya Malaika husujudia adhama yako, wakifurahi daima na milele mbele ya uso wako. Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukishiriki kusema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA“ZA MWAKA” IV: Historia ya wokovu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Maana yeye kwa kuzaliwa kwake alitengeneza upya ubinadamu uliochakaa, na kwa kuteswa alizifuta kabisa dhambi zetu; kwa kufufuka katika wafu alitupatia njia ya uzima wa milele, na kwa kupaa huko kwako, Ee Mungu Baba, aliyafungua malango ya mbinguni.
Kwa hiyo, sisi pamoja na umati wa Malaika na Watakatifu, tunakuimbia utenzi wa sifa, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA“ZA MWAKA” V: Kuumbwa ulimwengu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe ulivifanya vitu vyote vya ulimwengu, na ukapanga majira na nyakati. Ulimwumba mtu kwa mfano wako, na ukaweka chini yake viumbe na maajabu yao, apate kuvitawala, kwa niaba yako, vyote ulivyoviumba, na kukusifu bila mwisho katika maajabu ya kazi zako, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa hiyo, sisi nasi pamoja na Malaika wote tunakusifu, tukiimba kwa shangwe na furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA“ZA MWAKA” VI: Amana ya Pasaka ya milele.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Ndani yako tunaishi, tunajimudu na kuwa na uhai, na tukiwa katika mwili huu si tu tunaonja kila siku matokeo ya wema wako, bali pia tunayo tayari amana ya umilele. Kwa vile tunayo malimbuko ya Roho yule, ambaye kwa njia yake ulimfufua Yesu katika wafu, tunatumaini kwamba fumbo la Pasaka liwe kwetu la milele.
Kwa hiyo, sisi nasi pamoja na Malaika wote tunakusifu, tukiimba kwa shangwe na furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA"ZA MWAKA” VII: Wokovu kwa njia ya utii wake Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa maana Wewe jinsi hii uliupenda ulimwengu hata, kwa kutuhurumia, ukamtoa kwetu Mkombozi. Ulitaka aishi sawa na sisi, lakini bila dhambi, ili upate kupenda ndani yetu yale uliyokuwa unayapenda ndani ya Mwanao, ambaye kwa utii wake tumerudishiwa vipaji vyako, tulivyovipoteza kwa dhambi ya kutotii kwetu.
Kwa hiyo, ee Bwana, sisi nasi pamoja na Malaika na Watakatifu wote, tunakusifu, tukisema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

DOMINIKA "ZA MWAKA" VIII: Kanisa limekusanywa na umoja wa Utatu Mtakatifu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Maana, kwa damu ya Mwanao na nguvu za Roho Mtakatifu, ulipenda kuwakusanya tena kwako katika umoja wanao wote, ambao hatia ya dhambi iliwapeleka mbali nawe. Nao watu, waliokusanywa na umoja wa Utatu Mtakatifu, watambuliwe kuwa Kanisa, Mwili wa Kristo na Hekalu la Roho Mtakatifu, kwa sifa ya hekima yako iliyo ya namna nyingi.
Kwa hiyo, pamoja na Malaika wa mbinguni, tunakusifu tukiungama kwa furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

6. UTANGULIZI EKARISTI TAKATIFU
EKARISTI TAKATIFU I: Sadaka na sakramenti ya Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye aliye Kuhani wa kweli na wa milele, alipoweka utaratibu wa sadaka hii ya kudumu, alijitoa wa kwanza kwako kafara ya kuleta wokovu, akatuagiza na sisi tuitoe kwa kumkumbuka Yeye. Nasi tunaimarishwa, tupokeapo mwili wake uliotolewa sadaka kwa ajili yetu, na tunatakaswa, tuinywapo damu yake iliyomwagika kwa ajili yetu.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

EKARISTI TAKATIFU II: Matunda ya Ekaristi Takatifu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye alipokuwa anakula pamoja na Mitume wake katika karamu ya mwisho, alijitoa kwako kama Mwanakondoo asiye na doa, sadaka iliyokubalika ya kukusifu kikamilifu, ili kuudumisha kwa karne zote ukumbusho wa msalaba uletao wokovu. Kwa njia ya fumbo hili takatifu unawalisha na kuwatakatifuza waamini wako, ili wanadamu wote, walioenea katika dunia nzima, imani moja iwaangaze, na upendo mmoja uwaunganishe. Kwa hiyo sisi tunajongea meza ya sakramenti hii ya ajabu, ili, tukijazwa na wema wa neema yako, tugeuzwe kuwa na hali takatifu ya mbinguni.
Kwa sababu hiyo, viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani vinakuabudu vikiimba wimbo mpya; nasi pia, pamoja na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, tunakutukuza tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

7. UTANGULIZI BIKIRA MARIA
BIKIRA MARIA I: Umama wa Bikira Maria mwenye heri.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, na kukusifu, kukuhimidi na kukutangaza Wewe, katika adhimisho la sikukuu (katika adhimisho kwa heshima) ya Maria mwenye heri Bikira daima.
Yeye alimchukua mimba Mwanao pekee hapo Roho Mtakatifu alipomfunika kwa kivuli chake, na, pasipo kupoteza utukufu wa ubikira wake, aliuzalia ulimwengu mwanga wa milele, Yesu Kristo Bwana wetu. Kwa njia yake Malaika husifu adhama yako, Enzi hukuabudu, na Mamlaka hukupigia magoti wakitetemeka. Mbingu na Nguvu za mbinguni, na Maserafi wenye heri, wakuadhimisha pamoja kwa shangwe.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukisema kwa sauti ya unyenyekevu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

BIKIRA MARIA II: Kanisa humsifu Mungu kwa maneno ya Bikira Maria.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, kukukiri Wewe mtukufu kwa unayoyatenda katika Watakatifu wote, na hasa, tunapofanya kumbukumbu ya Bikira Maria mwenyeheri, kuitukuza huruma yako kwa utenzi wake mwenyewe wenye shukrani.
Kweli umetenda mambo makuu popote duniani, na ukaendeleza wingi wa rehema zako kwa karne na karne, pale ambapo, kwa kuutazama unyonge wa mjakazi wako, ulimtoa kwa njia yake mwanzilishi wa wokovu wa wanadamu, yaani Mwanao, Yesu Kristo Bwana wetu. Kwa njia yake majeshi ya Malaika husujudia adhama yako, wakifurahi daima na milele mbele ya uso wako.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukishiriki kusema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

8. UTANGULIZI MALAIKA
MALAIKA: Mungu hutukuzwa kwa njia ya Malaika.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Sisi hatukomi kukusifu katika Malaika wakuu na Malaika wako, kwa maana utukufu huifikia adhama yako tunapowaheshimu viumbe hao, Malaika wako, unaopendezwa nao. Nao, ingawa heshima na cheo chao ni kikubwa, wanadhihirisha jinsi Wewe ulivyo mkubwa zaidi, na inavyotakiwa usifiwe juu ya vitu vyote, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa njia yake wingi wa Malaika hutukuza adhama yako, nasi twajiunga nao katika kukuabudu kwa shangwe, tukiimba pamoja nao kwa sauti kuu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

9. UTANGULIZI MT. YOSEFU
MT. YOSEFU: Utume wa Mt. Yosefu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, na kukusifu kwa mbiu inayokustahili, na kukuhimidi na kukutangaza Wewe, katika adhimisho la sikukuu [katika adhimisho kwa heshima] ya Yosefu mwenye heri.
Yeye alikuwa mtu mwenye haki, uliyependa awe Mume wake Bikira Maria Mama wa Mungu; na, kama mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ulimweka juu ya Familia yako takatifu awe baba mlinzi wa Mwanao mpenzi, Yesu Kristo Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa njia yake Malaika husifu adhama yako, Enzi hukuabudu, na Mamlaka hukupigia magoti wakitetemeka. Mbingu na Nguvu za mbinguni, na Maserafi wenye heri, wakuadhimisha pamoja kwa shangwe.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukisema kwa sauti ya unyenyekevu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

10. UTANGULIZI MITUME
MITUME I: Mitume, wachungaji wa taifa la Mungu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe, Mchungaji wa milele, huliachi kundi lako, bali walilinda na kulitunza siku zote kwa njia ya Mitume wenye heri, lipate kuongozwa na mawakili walewale wa Mwanao uliowaweka kulisimamia kama wachungaji.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wako tukisema kwa sauti ya unyenyekevu.

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

MITUME II: Msingi na ushuhuda wa Mitume.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa maana ulipenda kuwaweka Mitume wawe misingi ya Kanisa lako, ili lidumu daima kuwa ishara ya utakatifu wako duniani, na kuwapatia watu wote ushuhuda wa mambo ya mbinguni.
Kwa sababu hiyo sasa na hata milele sisi pamoja na majeshi yote ya Malaika tunakuimbia kwa uchaji, tukipaza sauti na kusema:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

11. UTANGULIZI WATAKATIFU
WATAKATIFU I: Utukufu wa Watakatifu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe hutukuzwa katika kusanyiko la Watakatifu, na kwa kuwapa taji kwa mastahili yao unatuza mapaji yako. Wewe unatujalia mfano katika mwenendo wao, na ushirika katika kuungana nao, na msaada wa maombezi yao; ili, kwa kuthibitishwa na mashahidi wengi namna hii, tupige mbio bila kushindwa katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu na tupate pamoja nao lile taji la utukufu lisiloharibika, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, na umati mkubwa wa Watakatifu tunakuimbia utenzi wa sifa, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

WATAKATIFU II: Matendo ya Watakatifu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Wewe, kwa njia ya ushuhuda wa ajabu wa Watakatifu wako, unalisitawisha daima Kanisa kwa kulipatia nguvu mpya, na unatujalia sisi ishara za hakika za upendo wako. Lakini pia, sisi twahimizwa na mfano wao bora, na kusaidiwa siku zote na maombezi yao matakatifu, hadi mafumbo ya wokovu yatimizwe.
Kwa hiyo, ee Bwana, sisi nasi pamoja na Malaika na Watakatifu wote, tunakusifu, tukisema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

12. UTANGULIZI MASHAHIDI
MASHAHIDI I: Ishara na mfano wa Mashahidi.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa maana damu ya Mtakatifu J. Shahidi, iliyomwagwa ili kuungama jina lako kwa kumwiga Kristo, inadhihirisha maajabu yako. Kwa jinsi hiyo unakamilisha uweza katika udhaifu, na kuwapatia wasioweza nguvu za kutoa ushuhuda, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Nguvu za mbinguni, tunakutukuza daima hapa duniani tukisifu bila mwisho adhama yako kwa sauti kuu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

MASHAHIDI II: Maajabu ya Mungu katika ushindi wa Mashahidi.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa maana Wewe unatukuzwa katika sifa za Watakatifu wako, na matendo ya uweza wako ni ya ajabu katika yote yahusuyo mateso yao. Wewe unawajalia kwa wema ari ya imani hiyo, uthabiti katika udumifu, na ushindi katika mapambano, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa sababu hiyo, viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani vinakuabudu vikiimba wimbo mpya; nasi pia, pamoja na majeshi yote ya Malaika, tunakutukuza tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

13. UTANGULIZI WACHUNGAJI
WACHUNGAJI: Kuwepo kwa Wachungaji watakatifu katika Kanisa.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kia njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa kuwa, kama unavyolijalia Kanisa lako kuifurahia sikukuu ya Mtakatifu wako J., hali kadhalika unaliimarisha kwa mifano ya maisha yake matakatifu, unalifundisha kwa maneno ya mahubiri yake, na kulilinda kwa maombezi yake bora.
Kwa hiyo, sisi pamoja na umati wa Malaika na Watakatifu, tunakuimbia utenzi wa sifa, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

14. UTANGAULIZI MABIKIRA NA WATAWA
MABIKIRA NA WATAWA: Ishara ya maisha ya wakfu kwa Mungu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Maana katika Watakatifu, ambao walijitolea kwa Kristo kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, inafaa kuadhimisha maongozi yako ya ajabu. Kwa maongozi hayo unawarudisha wanadamu kwenye utakatifu wa asili, na kuwaongoza kuvionja hapa duniani vipaji vitakavyopatikana katika ulimwengu mpya.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Watakatifu na Malaika wote, tunakusifu, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

15. UTANGULIZI KAWAIDA
KAWAIDA I: Kufanywa upya kwa kila kitu katika Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa maana ulipenda kuvifanya upya vitu vyote katika Yeye, na kutujalia sisi kushiriki utimilifu wake. Maana, ingawa Yeye alikuwa Mungu, alijifanya kuwa hana utukufu, na kwa damu yake msalabani akavipatanisha naye vitu vyote. Kwa sababu hiyo ametukuzwa juu ya vitu vyote, naye akawa sababu ya wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na pamoja na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KAWAIDA II: Wokovu kwa njia ya Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe ulimwumba mtu kwa wema wako, na alipoadhibiwa kufa kwa mujibu wa haki, ulimkomboa kwa sababu ya huruma yako, kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Kwa njia yake Malaika husifu adhama yako, Enzi hukuabudu, na Mamlaka hukupigia magoti wakitetemeka. Mbingu na Nguvu za mbinguni, na Maserafi wenye heri, wakuadhimisha pamoja kwa shangwe.
Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukisema kwa sauti ya unyenyekevu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KAWAIDA III: Sifa kwa Mungu kwa sababu ya kuwaumba na kuwafanya upya wanadamu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe, kama vile ulivyowaumba wanadamu wote kwa njia ya Mwanao mpenzi, hali kadhalika katika yeye uliwafanya upya kwa wema mkuu. Kwa sababu hiyo, kwa haki viumbe vyote vinakutumikia, nao wote waliokombolewa nawe wanakusifu pamoja kwa ibada, na Watakatifu wako wanakuhimidi kwa moyo mmoja.
Kwa hiyo, sisi nasi pamoja na Malaika wote tunakuadhimisha, tukikukiri sikuzote kwa kuimba kwa furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KAWAIDA IV: Kumsifu Mungu ni kipaji cha Mungu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe huna haja na sifa yetu, lakini sifa hii ni kipaji chako tunachokurudishia kwa shukrani, maana, nyimbo zetu za sifa hazikuzidishii kitu, bali zatufaa sisi kupata wokovu, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa hiyo, pamoja na Malaika wa mbinguni, tunakusifu tukiungama kwa furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KAWAIDA V: Kutangaza fumbo la Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Tunaadhimisha kifo chake kwa mapendo, tunaungama ufufuko wake kwa imani hai, na kungojea kna matumaini thabiti ujio wake katika utukufu.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Watakatifu na Malaika wote, tunakusifu, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

KAWAIDA VI: Fumbo la wokovu katika Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Baba uliye mtakatifu, kwa njia ya Mwanao mpenzi, Yesu Kristo, Neno wako, ambaye kwa njia yake uliumba vitu vyote.
Ndiye uliyemtuma kwetu kama Mwokozi na Mkombozi, akafanyika mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira. Kwa kuwa alitaka kutimiza mapenzi yako na kukupatia taifa takatifu alipanua mikono yake alipoteswa msalabani, ili aangamize mauti na kudhihirisha ufufuko.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Watakatifu wote tunatangaza utukufu wako, tukisema kwa sauti moja:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

16. UTANGULIZI NDOA
MISA YA KUADHIMISHA SAKRAMENTI YA NDOA: Ndoa ni ishara ya mapendo ya kimungu.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Wewe ulimwumba mwanadamu kwa paji la wema wako, ukapenda kumwinua kwenye cheo kikubwa sana, ili katika muungano wa mume na mke upate kutuachia mfano halisi wa upendo wako. Naye uliyemwumba kwa mapendo yako, hukomi kumwita kwenye sheria ya mapendo, upate kumshirikisha mapendo yako ya milele. Sakramenti hii ya ndoa takatifu, kwa kuonesha ishara ya upendo wako, huutakatifuza upendo wa wanadamu, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Malaika na Watakatifu wote, tunakuimbia utenzi wa sifa, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

17. UTANGULIZI WAFU
WAFU I: Tumaini la ufufuko katika Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Katika Yeye tumaini la ufufuko wenye heri liliangaza kwetu, ili sisi, tunaosikitika kwa sababu tunajua kwamba lazima tutakufa, tufarijiwe kwa ahadi ya uzima wa milele. Maana, uzima wa waamini wako, ee Bwana, hauondolewi, ila unageuzwa tu, na hao wanapata makao ya milele mbinguni, yakiisha bomolewa makao ya hapa duniani.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Malaika Wakuu, pamoja na Viti vya enzi na Milki, na pamoja na majeshi yote ya Malaika wa mbinguni, twaimba utenzi wa utukufu wako, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

WAFU II: Kristo alikufa ili sisi tupate uzima.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye ndiye yule mmoja aliyepokea mauti, ili sisi sote tusije tukafa; ila mmoja tu alikubali kufa, kusudi sote tupate kuishi kwa ajili yako milele.
Kwa hiyo, pamoja na Malaika wa mbinguni, tunakusifu tukiungama kwa furaha:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

WAFU III: Kristo ndiye wokovu na uzima.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Yeye ndiye wokovu wa ulimwengu, uzima wa wanadamu, ufufuko wa wafu.
Kwa njia yake majeshi ya Malaika husujudia adhama yako, wakifurahi daima na milele mbele ya uso wako. Tunakusihi, utujalie tujiunge nao kwa wimbo wa sifa, tukishiriki kusema kwa shangwe:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

WAFU IV: Kutoka maisha ya duniani kufika kwenye utukufu wa mbinguni.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Kwa amri yako twazaliwa. kwa matakwa yako twaongozwa, na kwa agizo lako tunakombolewa na sheria ya dhambi, inayoturudisha katika udongo, ambamo tulichukuliwa kwanza. Nasi tuliokombolewa kwa njia ya kifo cha Mwanao, kwa ishara yako tunaamshwa kwenye utukufu wa ufufuko wake.
Kwa hiyo, sisi pamoja na umati wa Malaika na Watakatifu, tunakuimbia utenzi wa sifa, tukisema bila mwisho:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

WAFU V: Ufufuko wetu huja kwa ushindi wa Kristo.
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Bwana, Baba uliye mtakatifu, Mungu mwenyezi wa milele.
Ingawa tunastahili kufa, lakini unatuhurumia kwa neema yako kwamba, tukiisha kuangamizwa na mauti kwa sababu ya dhambi, tunakombolewa kwa njia ya ushindi wa Kristo, na kuitwa tena pamoja naye kwenye uzima.
Kwa hiyo, sisi pamoja na Nguvu za mbinguni, tunakutukuza daima hapa duniani tukisifu bila mwisho adhama yako kwa sauti kuu:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

---------

SALA YA EKARISTI I
(KANUNI YA KIROMA)

Kuhani, hali amefumbua mikono, anasema:
KK.
Ee Baba mwingi wa huruma, tunakusihi kwa unyenyekevu na kukuomba kwa njia ya Yesu Kristo, Mwanao, Bwana wetu,

anafumba mikono na kusema:
uvipokee

na kufanya ishara ya msalaba mara moja tu juu ya mkate na kalisi, akisema:
na kuvibariki + vipaji hivi,
sadaka hizi, dhabihu hizi takatifu na safi,
tunazokutolea kwanza kabisa
kwa ajili ya Kanisa lako takatifu katoliki.
Ukubali kuliletea amani, kulilinda,
kulikusanya katika umoja
na kuliongoza popote duniani,
pamoja na mtumishi wako
Baba Mtakatifu wetu J. na Askofu wetu J.,
na wote wenye kushika imani ya kweli, katoliki na ya Mitume.

Kuwakumbuka waamini walio hai.
K1.
Ee Bwana, uwakumbuke
watumishi wako J. na J.

Anafumba mikono na kusali kidogo kwa ajili ya wale anaokusudia kuwaombea. Halafu, hali amefumbua mikono, anaendelea kusema:
nao wote waliopo hapa, ambao wewe waijua imani na ibada yao.

Kwa ajili yao tunakutolea dhabihu hii ya sifa, nao wenyewe wanakutolea dhabihu hiyo, kwa ajili yao na kwa ajili ya jamaa zao wote, kwa ukombozi wa roho zao, katika tumaini la kupata wokovu na usalama, na wanatolea nadhiri zao kwako wewe Mungu wa milele, uliye hai na wa kweli.

------------------
KWA KUSHIRIKIANA ZA PEKEE
Noeli na Oktava yake

Kwa kushirikiana na Kanisa zima, katika kuadhimisha
(ule usiku mtakatifu sana) ile siku takatifu sana,
Maria mwenye heri daima Bikira alipoizalia dunia hii Mwokozi; tunamkumbuka kwanza na kumheshimu huyo Maria mtukufu daima Bikira, Mama wa huyo Yesu Kristo, Mungu na Bwana wetu;

Epifania ya Bwana
katika kuadhimisha ile siku takatifu sana, ambapo Mwanao pekee, aliye wa milele pamoja nawe katika utukufu wako, alitokea na kuonekana wazi katika mwili, akishiriki kweli ubinadamu wetu; tunamkumbuka kwanza na kumheshimu Maria mtukufu daima Bikira, Mama wa Mungu na Bwana wetu, Yesu Kristo;

Kuanzia Misa ya Kesha la Pasaka hadi Dominika ya 2 ya Pasaka
Kwa kushirikiana na Kanisa zima, katika kuadhimisha (ule usiku mtakatifu sana wa)
ile siku takatifu sana ya -Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo katika mwili, tunamkumbuka kwanza na kumheshimu Maria mtukufu daima Bikira, Mama wa Mungu na Bwana wetu, Yesu Kristo;

Kupaa kwake Bwana
Kwa kushirikiana na Kanisa zima, katika kuadhimisha ile siku takatifu sana, ambapo Bwana wetu, Mwanao pekee, aliuweka kuume kwako katika utukufu ubinadamu wetu dhaifu akiisha kuuunganisha naye, tunamkumbuka kwanza na kumheshimu Maria mtukufu daima Bikira, Mama wa Mungu na Bwana wetu, Yesu Kristo;

Dominika ya Pentekoste
Kwa kushirikiana na Kanisa zima, katika kuadhimisha siku takatifu sana ya Pentekoste, ambapo Roho Mtakatifu, aliwatokea Mitume katika ndimi za moto; tunamkumbuka kwanza na kumheshimu
Maria mtukufu daima Bikira, Mama wa Mungu na Bwana wetu, Yesu Kristo:

---------------

K2. Kwa kushirikiana na Kanisa zima,
tunamkumbuka kwanza na kumheshimu
Maria mtukufu daima Bikira,
Mama wa Yesu Kristo Mungu Bwana wetu;

halafu Yosefu mwenye heri, Mume wake huyo Bikira, na Mitume na Mashahidi wako wenye heri, Petro na Paulo, Andrea,
(Yakobo, Yohane, Tomaso, Yakobo, Filipo, Bartolomayo, Matayo, Simoni na Tadayo; Lino, Kleto, Klementi, Sisto, Kornelio, Sipriano, Laurenti, Krisogoni, Yohane na Paulo, Kosma na Damiano)
na Watakatifu wako wote. Kwa mastahili na maombezi yao utujalie tuimarishwe katika mambo yote kwa msaada wa ulinzi wako.

(Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.)

Hali amefumbua mikono, anaendelea kusema:
KK. Kwa hiyo, ee Bwana, tunakuomba upokee kwa wema sadaka hii tunayokutolea sisi watumishi wako, na familia yako yote. Na uziweke siku zetu katika amani yako, na uamuru tuopolewe kutoka laana ya milele na tuhesabiwe katika kundi la wateule wako.

Anafumba mikono.
(
Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.)

---------------------
Kuanzia Misa ya Kesha la Pasaka hadi Dominika ya 2 ya Pasaka
Kwa hiyo, ee Bwana, tunakuomba upokee kwa wema sadaka hii tunayokutolea sisi watumishi wako, na familia yako yote. Tunakutolea pia kwa ajili ya hao uliopenda wazaliwe upya kwa maji na Roho Mtakatifu, kwa kuwajalia ondoleo la dhambi zao zote. Na uziweke siku zetu katika amani yako, na uamuru tuopolewe kutoka laana ya milele na tuhesabiwe katika kundi la wateule wako.

Anafumba mikono.
(Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.)

------------------------
Huku akiitandaza mikono juu ya mkate na divai, anasema:
KW.
Ewe Mungu, tunakuomba, uibariki sadaka hii, ikupendeze, uipokee, iwe sadaka yenye maana, na inayokubalika katika yote: ili iwe kwetu Mwili na Damu ya Mwanao mpendwa sana, Bwana wetu Yesu Kristo.

Anafumba mikono.
Yeye, siku iliyotangulia kuteswa kwake, alitwaa mkate katika mikono yake mitakatifu na mitukufu, akainua macho mbinguni kwako wewe Mungu, Baba yake mwenyezi, akikushukuru, aliubariki, akaumega, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MLE NYOTE:
HUU NDIO MWILI WANGU,
UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU.

Anawaonesha waamini hostia takatifu, na kuiweka kwenye Patena, na, kwa kupiga goti, anaabudu.
Vivyo hivyo, baada ya kula, akitwaa kikombe hiki kitukufu katika mikono yake mitakatifu na mitukufu, akikushukuru tena, alikibariki, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MNYWE NYOTE:
HIKI NDICHO KIKOMBE CHA DAMU YANGU,
DAMU YA AGANO JIPYA NA LA MILELE.
ITAKAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU
NA KWA AJILI YA WENGI
KWA MAONDOLEO YA DHAMBI.
FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.

Anawaonesha waamini kalisi, anaiweka juu ya korporale, na, akipiga goti, anaabudu. Halafu anasema:
KK. Fumbo la imani.
W. Ee Bwana, tunatangaza kifo chako, na kutukuza ufufuko wako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Bwana, kila tunapokula mkate huu na kukinywea kikombe hiki, tunatangaza kifo chako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Mwokozi wa ulimwengu, utuokoe, Wewe uliyetukomboa kwa msalaba na ufufuko wako.

KW. Kwa hiyo, ee Bwana,
sisi watumishi wako, na taifa lako takatifu, tunaadhimisha ukumbusho wa mateso matakatifu ya huyo Kristo Mwanao Bwana wetu, pamoja na ufufuko wake kutoka kuzimu, na kupaa kwake mbinguni kwa utukufu.

Tunakutolea wewe, ee Mungu Mtukufu na mwenye enzi, kati ya zawadi ulizotujalia, sadaka safi, sadaka takatifu, sadaka isiyo na mawaa, Mkate mtakatifu wa uzima wa milele na Kikombe cha wokovu wa milele.

Uwe radhi kuitazama sadaka hii kwa uso wa huruma na wema: uipokee, kama ulivyokubali kupokea sadaka yake Abeli, mtumishi wako mwenye haki, na dhabihu ya Babu yetu Ibrahimu, na ile aliyokutolea Melkisedeki, kuhani wako mkuu, kama dhabihu takatifu, sadaka isiyo na mawaa.

Hali akiinama, na kufumba mikono, anaendelea kusema:
Ee Mungu mwenyezi, tunakuomba kwa unyenyekevu, amuru kwamba sadaka hii ichukuliwe kwa mikono ya Malaika wako mtakatifu na kupelekwa mpaka kwenye altare yako juu mbinguni, mbele ya uso wako mtukufu, kusudi, sisi sote tutakaopokea Mwili na Damu takatifu ya Mwanao kwa kushiriki katika altare hii,

anainuka na kupiga ishara ya msalaba, akisema:
tujazwe kila baraka na neema ya mbinguni.

Anafumba mikono.
(Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.)

Akifumbua mikono, anasema:
K3.
Ee Bwana, uwakumbuke pia watumishi wako J. na J., waliotutangulia wakiwa na ishara ya imani, wamepumzika katika usingizi wa amani.

Tunakusihi, ee Bwana, uwajalie mahali pa faraja, mwanga na amani, hao na wote wanaopumzika katika Kristo.

Anafumba mikono.
(Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.)

Akijipiga kifua kwa mkono wake wa kulia, anasema:
Nasi pia watumishi wako wakosefu,

Na, akiisha kufumbua mikono, anaendelea kusema:
tunaotumainia wingi wa rehema zako, utujalie sehemu ya urithi na ushirika pamoja na Mitume na Mashahidi wako watakatifu; pamoja na Yohane, Stefano, Matia, Barnaba;
(Ignasi, Aleksanda, Marselino, Petro, Felisita, Perpetua, Agata, Lusia, Agnesi, Sesilia, Anastasia)
na Watakatifu wako wote.

Tunakuomba, ee Mungu Mkarimu, utupokee na sisi katika ushirika wao, si kwa kuhesabu mastahili yetu, bali kwa ajili ya msamaha wako.

Anafumba mikono.
(Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.)

KK. Ee Bwana, kwa njia yake,
unaumba daima mema hayo yote, unayatakatifuza, kuyatia uzima, kuyabariki na kutujalia sisi.

Anatwaa patena yenye hostia takatifu na kalisi, na akiivinua vyote viwili, anasema:
Kwa njia yake,
na pamoja naye na ndani yake,
wewe, Mungu Baba mwenyezi,
katika umoja wa Roho Mtakatifu,
unapata heshima yote na utukufu
milele na milele.

W. Amina.

-------------

SALA YA EKARISTI II

UTANGULIZI
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema na haki, tendo la kufaa na la kuleta wokovu, tukushukuru Wewe daima na popote, ee Baba uliye mtakatifu, kwa njia ya Mwanao mpenzi, Yesu Kristo, Neno wako, ambaye kwa njia yake uliumba vitu vyote.
Ndiye uliyemtuma kwetu kama Mwokozi na Mkombozi, akafanyika mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira. Kwa kuwa alitaka kutimiza mapenzi yako na kukupatia taifa takatifu alipanua mikono yake alipoteswa msalabani, ili aangamize mauti na kudhihirisha ufufuko.
Kwa sababu hiyo, sisi pamoja na Malaika na Watakatifu wote tunatangaza utukufu wako, tukisema kwa sauti moja:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

kuhani, hali amefumbua mikono, anasema.
KK. Ee Bwana, kweli u Mtakatifu, na chemchemi ya utakatifu wote.

Anafumba mikono, na kuitandaza juu ya mkate na divai, akisema:
KW. Tunakuomba uvitakatifuze vipaji hivi kwa nguvu ya Roho wako,

Anafumba mikono, na kufanya ishara ya msalaba mara moja tu juu ya mkate na kalisi, akisema:
ili viwe kwetu Mwili na + Damu
ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Anafumba mikono.
Yeye alipotolewa na kuingia kwa hiari katika Mateso yake,
alitwaa mkate, akashukuru, akaumega, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MLE NYOTE:
HUU NDIO MWILI WANGU,
UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU.

Anawaonesha waamini hostia takatifu, na kuiweka kwenye Patena, na, kwa kupiga goti, anaabudu.
Vivyo hivyo, baada ya kula,
akitwaa kikombe,
na kukushukuru tena,
aliwapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MNYWE NYOTE:
HIKI NDICHO KIKOMBE CHA DAMU YANGU,
DAMU YA AGANO JIPYA NA LA MILELE,
ITAKAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU
NA KWA AJILI YA WENGI
KWA MAONDOLEO YA DHAMBI.
FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.

Anawaonesha waamini kalisi, anaiweka juu ya korporale, na, akipiga goti, anaabudu. Halafu anasema:
KK. Fumbo la imani.
W. Ee Bwana, tunatangaza kifo chako, na kutukuza ufufuko wako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Bwana, kila tunapokula mkate huu na kukinywea kikombe hiki, tunatangaza kifo chako, mpaka utakapokuja.

Au.
W.
Ee Mwokozi wa ulimwengu, utuokoe, Wewe uliyetukomboa kwa msalaba na ufufuko wako.

Halafu kuhani, hali amefumbua mikono, anasema:
Kwa hiyo, ee Bwana, tunapoadhimisha ukumbusho wa kifo na ufufuko wake Mwanao, tunakutolea mkate wa uzima na kikombe cha wokovu.

Tunakushukuru kwa kuwa umetustahilisha kusimama mbele yako na kukutumikia. Pia tunakusihi kwa unyenyekevu ili, kwa kushiriki Mwili na Damu ya Kristo, tukusanywe na Roho Mtakatifu tupate kuwa jamaa moja.

K1. Ee Bwana, ulikumbuke Kanisa lako lililoenea popote duniani, ulikamilishe katika mapendo, pamoja na Baba mtakatifu wetu J. na Askofu wetu J., na Waklero wote.

--------------
Katika Misa kwa wafu inawezekana kuongeza:
Umkumbuke mtumishi wako J., uliyemwita kwako (leo) kutoka dunia hii. Ujalie, ili, yeye aliyeshirikishwa kifo cha Mwanao kwa Ubatizo, ashiriki pia ufufuko wake.
----------------

K2. Uwakumbuke pia ndugu zetu, waliofariki dunia wakiwa na tumaini la ufufuko, na marehemu wote, waliofariki dunia katika huruma yako, uwapokee kwenye nuru ya uso wako.

K3. Tunakuomba, utuhurumie sisi sote, ili, pamoja na Maria Bikira mwenye heri Mama wa Mungu, na mtakatifu Yosefu, mume wake huyo Bikira, Mitume wenye heri na Watakatifu wote waliokupendeza tangu kale, tustahili kushiriki uzima wa milele, na kukusifu na kukutukuza

anafumba mikono
kwa njia ya Mwanao Yesu Kristo.

Anatwaa patena yenye hostia takatifu na kalisi, na akiviinua vyote viwili, anasema:
Kwa njia yake,
na pamoja naye na ndani yake,
wewe, Mungu Baba mwenyezi,
katika umoja wa Roho Mtakatifu,
unapata heshima yote na utukufu
milele na milele.

W. Amina.

------------

SALA YA EKARISTI III

Kuhani, hali amefumbua mikono, anasema:
KK.
Ee Bwana, kweli u Mtakatifu, na kila kiumbe kilichoumbwa nawe kinakusifu kwa haki. Maana, kwa njia ya Mwanao, Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa uwezo tendaji wa Roho Mtakatifu, unavitia uzima vitu vyote na kuvitakatifuza, wala huachi kukusanya watu kwako, ili, toka maawio ya jua hata machweo yake, dhabihu safi itolewe kwa jina lako.

Anafumba mikono, na kuitandaza juu ya mkate na divai, akisema:
KW. Basi, ee Bwana, tunakusihi kwa unyenyekevu, vipaji hivi, ambavyo tumekutolea ili uvitakase, upende kuvitakatifuza kwa Roho huyo huyo,

anafumba mikono na kufanya ishara ya msalaba mara moja tu juu ya mkate na kalisi, akisema:
ili viwe Mwili na + Damu
ya Mwanao, Bwana wetu Yesu Kristo,

anafumba mikono
aliyetuamuru tuadhimishe mafumbo haya.

Maana, Yeye mwenyewe, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, na akikushukuru, aliubariki, akaumega, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MLE NYOTE:
HUU NDIO MWILI WANGU,
UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU.

Anawaonesha waamini hostia takatifu, na kuiweka kwenye patena, na, akipiga goti, anaabudu. Halafu anaendelea akisema:
Vivyo hivyo, baada ya kula,
akitwaa kikombe, na kukushukuru, alikibariki, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MNYWE NYOTE:
HIKI NDICHO KIKOMBE CHA DAMU YANGU,
DAMU YA AGANO JIPYA NA LA MILELE,
ITAKAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU
NA KWA AJILI YA WENGI
KWA MAONDOLEO YA DHAMBI.
FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.

Awaonesha waamini kalisi, anaiweka juu ya korporale, na, akipiga goti, anaabudu.

KK. Fumbo la imani.
W. Ee Bwana, tunatangaza kifo chako, na kutukuza ufufuko wako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Bwana, kila tunapokula mkate huu na kukinywea kikombe hiki, tunatangaza kifo chako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Mwokozi wa ulimwengu, utuokoe, Wewe uliyetukomboa kwa msalaba na ufufuko wako.

KW. Kwa hiyo, ee Bwana, tunapoadhimisha ukumbusho wa mateso ya Mwanao yaletayo wokovu, pamoja na ufufuko wake wa ajabu na kupaa kwake mbinguni, na tunapoutazamia ujio wake wa pili, tunakutolea, kwa shukrani, sadaka hii iliyo hai na takatifu.

Tunakuomba, uyaangalie matoleo ya Kanisa lako, na kwa kumtambua Yeye, aliye Kafara ambaye ulitaka kutulizwa kwa sadaka ya kifo chake, utujalie sisi tunaotiwa nguvu kwa Mwili na Damu ya Mwanao, na kujazwa Roho wake Mtakatifu, tupate kuwa mwili mmoja na roho moja katika Kristo.

K1. Yeye atufanye sisi tuwe kwako sadaka timilifu ya milele, ili tuweze kupata urithi pamoja na wateule wako: kwanza kabisa pamoja na Bikira Maria, mwenye heri, Mama wa Mungu, na mtakatifu Yosefu, mume wake huyo Bikira, na Mitume wako wenye heri na Mashahidi wako watukufu, (pamoja na Mtakatifu J.: Mtakatifu wa siku au Msimamizi) na Watakatifu wote, ambao tunategemea kupata daima msaada wa maombezi yao mbele zako.

K2. Tunakuomba, ee Bwana, huyu aliye Kafara na upatanisho wetu alete amani na wokovu duniani kote. Upende kuliimarisha katika imani na mapendo Kanisa lako, linalosafiri hapa duniani, pamoja na mtumishi wako Baba Mtakatifu wetu J. na Askofu wetu J., pamoja na Maaskofu wote, Waklero wote, na watu wote unaowafanya kuwa taifa lako.

K3. Usikilize kwa wema sala za jamaa hii uliyoiita hapa mbele yako. Ee Baba uliye mtakatifu, kwa huruma yako uwakusanye kwako wanao wote waliotawanyika popote duniani.

-------

--------
Uwapokee kwa wema katika ufalme wako ndugu zetu marehemu na wote walioaga dunia wakiwa wamekupendeza. Nasi tunatumaini kufika katika ufalme huo ili pamoja tushibishwe milele kwa utukufu wako,

Anafumba mikono
kwa njia ya Kristo Bwana wetu, ambaye kwa njia yake unaujalia ulimwengu mema yote.

Anatwaa patena yenye hostia takatifu na kalisi, na akiviinua vyote viwili, anasema:
Kwa njia yake,
na pamoja naye na ndani yake,
Wewe, Mungu Baba mwenyezi,
katika umoja wa Roho Mtakatifu,
unapata heshima yote na utukufu
milele na milele.

W. Amina.

------------
Iwapo Sala hii ya Ekaristi inatumiwa katika Misa kwa wafu, inawezekana kusema maneno haya:
Umkumbuke mtumishi wako J., uliyemwita kwako (leo) kutoka dunia hii. Umjalie kwamba, yeye ambaye alishirikishwa kifo cha Mwanao kwa Ubatizo, hali kadhalika ashiriki ufufuko wake, siku ambapo atawafufua wafu katika miili yao kutoka ardhini. Hapo, ataufananisha mwili wa unyonge wetu na mwili wa utukufu wake.

Pia uwapokee kwa wema katika ufalme wako ndugu zetu marehemu na wote walioaga dunia wakiwa wamekupendeza.

Nasi tunatumaini kufika katika ufalme huo ili pamoja tushibishwe milele kwa utukufu wako. Ndipo utakapofuta kila chozi katika macho yetu; maana kwa kukuona wewe, Mungu wetu, kama ulivyo, tutafanana nawe milele yote, na tutakusifu bila mwisho,

Anafumba mikono
kwa njia ya Kristo Bwana wetu, ambaye kwa njia yake unaujalia ulimwengu mema yote.

Anatwaa patena yenye hostia takatifu na kalisi, na akiviinua vyote viwili, anasema:
Kwa njia yake,
na pamoja naye na ndani yake,
wewe, Mungu Baba mwenyezi,
katika umoja wa Roho Mtakatifu,
unapata heshima yote na utukufu
milele na milele.

W. Amina.

------------

SALA YA EKARISTI IV

UTANGULIZI
Utangulizi wa Sala hii ya Ekaristi haubadiliki kwa sababu ya muundo wa Sala yenyewe, ambayo inaonesha muhtasari mkamilifu wa historia ya wokovu.

K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Inueni mioyo.
W. Tumeiinua kwa Bwana.
K. Tumshukuru Bwana Mungu wetu.
W. Ni vema na haki.

K. Kweli ni vema kukushukuru, pia ni haki kukutukuza, ee Baba uliye mtakatifu, kwa kuwa ndiwe peke yako Mungu mwenye uhai na wa kweli, uliye kabla ya nyakati zote na kudumu milele, unayeishi katika nuru isiyoweza kukaribiwa.
Wewe, uliye peke yako mwema na chemchemi ya uzima, umeviumba vitu vyote, ili kuvijaza baraka zako na kuvifurahisha kwa mng'ao wa nuru yako. Kwa hiyo makundi yasiyohesabika ya Malaika wanasimama mbele yako, na kukutumikia mchana na usiku, na, wakiukazia macho utukufu wa uso wako, wanakutukuza bila mwisho.
Nasi pia pamoja nao, na, kwa sauti zetu, pia viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu, tunalisifu kwa shangwe jina lako, tukiimba:

W. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu wa majeshi.
Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako.
Hosana juu mbinguni.
Mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.
Hosana juu mbinguni.

Kuhani, hali amefumbua mikono, anasema:
KK. Tunakusifu, ee Baba uliye mtakatifu, kwa kuwa u mkuu, na kazi zako zote umezifanya kwa hekima na upendo. Ulimwumba mtu kwa mfano wako, na kumkabidhi kuutunza ulimwengu wote, ili, anapokutumikia Wewe peke yako, uliye Muumba, avitawale viumbe vyote.

Naye, alipoupoteza urafiki wako kwa kutotii, hukumwacha katika utawala wa mauti. Maana, kwa huruma yako ulikuja kuwasaidia watu wote, ili wanaokutafuta wakupate. Zaidi ya hayo, mara nyingi ulifanya maagano na watu, na kwa njia ya manabii ukawafundisha kutazamia wokovu.

Na hivi, ee Baba uliye mtakatifu, jinsi hii uliupenda ulimwengu, hata ulipowadia utimilifu wa nyakati ukamtuma kwetu Mwanao wa pekee awe Mwokozi.

Yeye alifanyika mtu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Katika mambo yote alitwaa namna ya hali yetu, isipokuwa hakuwa na dhambi.

Aliwahubiria maskini habari njema ya wokovu, akawatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na wenye huzuni furaha. Ili apate kutimiza kabisa mpango wako wa ukombozi, alijitoa mwenyewe afe, naye, alipofufuka kutoka wafu, akaangamiza mauti na kuleta uzima upya.

Na kusudi tusiishi tena kwa ajili yetu sisi wenyewe, bali kwa ajili yake Yeye aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu, alimtuma Roho Mtakatifu kutoka kwako, ee Baba, awe malimbuko kwa waamini, ili aitimize kazi yake Mwanao ulimwenguni, na kukamilisha kazi yote ya kutakatifuza.

Anafumba mikono, na kuitandaza juu ya mkate na divai, akisema:
KW.
Kwa hiyo, ee Bwana, tunakuomba huyo Roho Mtakatifu apende kuvitakatifuza vipaji hivi,

anafumba mikono, na kufanya ishara ya msalaba mara moja tu juu ya mkate na kalisi, akisema:
ili viwe Mwili na + Damu
ya Bwana wetu Yesu Kristo

anafumba mikono
kwa ajili ya kuadhimisha fumbo hili kuu alilotuachia liwe agano la milele.

Maana, Yeye mwenyewe, ilipofika saa ya kutukuzwa nawe, ee Baba uliye mtakatifu, akiwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, aliwapenda upeo.

Walipokuwa wakila,

anatwaa mkate, na kwa kuuinua kidogo juu ya altare, anaendelea kutamka:
alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MLE NYOTE:
HUU NDIO MWILI WANGU,
UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU.

Anawaonesha waamini hostia takatifu, na kuiweka kwenye patena, na, akipiga goti, anaabudu. Halafu anaendelea akisema:
vivyo hivyo
akatwaa kikombe, kilichojaa divai, akashukuru, na akawapa wafuasi wake, akisema:

TWAENI, MNYWE NYOTE:
HIKI NDICHO KIKOMBE CHA DAMU YANGU.
DAMU YA AGANO JIPYA NA LA MILELE,
ITAKAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU
NA KWA AJILI YA WENGI
KWA MAONDOLEO YA DHAMBI.
FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU.

Anawaonesha waamini kalisi, anaiweka juu ya korporale, na, akipiga goti, anaabudu.
KK. Fumbo la imani.
W. Ee Bwana, tunatangaza kifo chako, na kutukuza ufufuko wako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Bwana, kila tunapokula mkate huu na kukinywea kikombe hiki, tunatangaza kifo chako, mpaka utakapokuja.

Au:
W.
Ee Mwokozi wa ulimwengu, utuokoe, Wewe uliyetukumboa kwa msalaba na ufufuko wako.

KW. Kwa hiyo, ee Bwana, tunapoadhimisha sasa ukumbusho wa ukombozi wetu, tunakumbuka kufa kwake Kristo na kushuka kwake kuzimu; tunatangaza pia kufufuka kwake na kupaa kwake mbinguni na kukaa kulia kwako.

Nasi tunapongojea kuja kwake katika utukufu, tunakutolea Mwili na Damu yake, iliyo sadaka ya kukupendeza, iletayo wokovu kwa ulimwengu wote.

Ee Bwana, umtazame huyu Kafara, ambaye ulimwandaa mwenyewe kwa ajili ya Kanisa lako.

Kwa wema wako uwajalie wote watakaoshiriki mkate huu mmoja na kikombe hiki, wakiisha kukusanywa katika mwili mmoja na Roho Mtakatifu, waweze kuwa dhabihu iliyo hai katika Kristo, kwa sifa ya utukufu wako.

K1. Sasa, ee Bwana, uwakumbuke wote ambao kwa ajili yao tunakutolea sadaka hii: kwanza kabisa mtumishi wako, Baba mtakatifu wetu J., Askofu wetu J., na Maaskofu wote; pamoja na Waklero wote, na wote wanaokutolea sadaka hii, na hawa waliopo hapa, na taifa lako lote, na watu wote wenye kukutafuta kwa moyo mnyofu.

K2. Uwakumbuke pia wale waliofariki dunia katika amani ya Kristo wako, na marehemu wote, ambao imani yao uliijua wewe peke yako.

Ee Baba uliye mtakatifu, utujalie sisi sote wanao, tuweze kupata urithi wa mbinguni katika ufalme wako, pamoja na Bikira Maria mwenye heri, Mama wa Mungu, mtakatifu Yosefu, mume wake huyo Bikira, na Mitume na Watakatifu wako.

Na huko mbinguni tukutukuze pamoja na viumbe vyote, vikiisha kuokolewa katika uharibifu wa dhambi na mauti, kwa njia ya Kristo Bwana wetu,

anafumba mikono,
ambaye kwa njia yake unaujalia ulimwengu mema yote.

Anatwaa patena yenye hostia takatifu na kalisi, na akiviinua vyote viwili, anasema:
Kwa njia yake,
na pamoja naye na ndani yake,
wewe, Mungu Baba mwenyezi,
katika umoja wa Roho Mtakatifu,
unapata heshima yote na utukufu
milele na milele.

W. Amina.

C. KOMUNYO

Baada ya kuweka altareni kalisi na patena, kuhani, hali amefumba mikono, anasema:
Kwa kulitii agizo la Mwokozi wetu, na tukifuata mafundisho yake ya kimungu, tunathubutu kusema:

Anafumbua mikono na anaendelea kusema, pamoja na waamini:
Baba yetu, uliye mbinguni, jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike; utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni.

amefumbua mikono:
KK. Ee Bwana, tunakuomba utuopoe katika maovu yote, utujalie kwa wema amani maishani mwetu, kusudi, kwa msaada wa huruma yako, tuopolewe daima na dhambi wala tusifadhaishwe na jambo lolote, tunapotazamia tumaini lenye heri, na ujio wa Mwokozi wetu Yesu Kristo.

W. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.

amefumbua mikono
KK. Ee Bwana Yesu Kristo, uliyewaambia Mitume wako, “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa”,usizitazame dhambi zetu, ila tu imani ya Kanisa lako; upende kulijalia amani na umoja, kama yalivyo mapenzi yako.

Anafumba mikono.
Unayeishi na kutawala milele na milele.

W. Amina.

huku akifumbua na kufumba mikono, anaendelea kusema:
KK.
Amani ya Bwana iwe daima nanyi.

W. Na iwe rohoni mwako.

KK. Mpeane amani.

Kisha, anachukua hostia takatifiu na kuimega juu ya patena, halafu anakitia kipande ndani ya kalisi, akisema kwa sauti isiyosikika:
KK. Huku kuchanganya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo kutupatie uzima wa milele sisi tunaopokea.

MWANAKONDOO
Mwanakondoo wa Mungu,
uondoaye dhambi za ulimwengu: utuhurumie.
Mwanakondoo wa Mungu,
uondoaye dhambi za ulimwengu: utuhurumie.
Mwanakondoo wa Mungu,
uondoaye dhambi za ulimwengu: utujalie amani.

Halafu kuhani, hali amefumba mikono, anasema kwa sauti isiyosikika:
KK.
Ee Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, kadiri ya mapenzi ya Baba, na kwa kutenda kazi pamoja na Roho Mtakatifu, uliupatia ulimwengu uzima kwa njia ya kifo chako. Uniokoe kwa Mwili na kwa Damu yako hii takatifu sana, katika maovu yangu yote na mabaya yote; unifanye niambatane daima na amri zako, wala usiruhusu nitengane nawe kamwe.

Au:
Ee Bwana Yesu Kristo, huku kupokea Mwili na Damu yako kusiwe kwangu hukumu na adhabu, bali, kwa huruma yako, kunifae mimi kwa kunilinda akili na mwili na kuwa dawa ya kuniponya.

Kuhani anapiga goti, halafu anachukua hostia takatifu na kuiinua kidogo juu ya patena au juu ya kalisi, na, akiwaelekea waamini, anasema kwa sauti ya kusikika:

KK. Tazama, Mwanakondoo wa Mungu, tazama, aondoaye dhambi za ulimwengu. Heri yao walioalikwa kwenye karamu ya Mwanakondoo.

Na anaendelea kusema, pamoja na waamini:
Ee Bwana, sistahili uingie kwangu, lakini sema neno tu, na roho yangu itapona.

Na kuhani, akiielekea altare, anasema kwa sauti ndogo:
KK.
Mwili wa Kristo unilinde nipate uzima wa milele.

Na kwa heshima anakula Mwili wa Kristo. Halafu anatwaa kalisi na kusema kwa sauti ndogo:
KK. Damu ya Kristo inilinde nipate uzima wa milele.

Na kwa heshima anakunywa Damu ya Kristo. Halafu anatwaa patena au siborio na anakwenda kukomunisha waamini, akiinua kidogo hostia na kumwonesha kila anayepokea, na kumwambia:

Mwili wa Kristo.

Mwenye kukomunika anaitikia:
Amina.

wakati vyombo vikiendelea kusafishwa, kuhani anasema kwa sauti isiyosikika:
Ee Bwana, tulichopokea kinywani, tukishike kwa moyo safi; na tulichopewa kama zawadi hapa duniani kiwe kwetu dawa ya kutuponya milele.

SALA BAADA YA KUMONYO

Akiwa amewaelekea waamini na mikono imefumbwa, anasema:
Tuombe.

Sala tazama link ya masomo hapo chini

W. Amina.

MWISHO WA ADHIMISHO

Anawaelekea waamini, akiwa amefumbua mikono, na kusema:
K. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
K. Awabariki Mungu mwenyezi, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
W. Amina.

--------
Askofu. Bwana awe nanyi.
W. Na awe rohoni mwako.
Askofu. Jina la Bwana litukuzwe.
W. Tangu sasa na hata milele.
Askofu. Msaada wetu u katika jina la Bwana.
W. Aliyezifanya mbingu na dunia.

Halafi Mwadhimishaji mkuu anapokea bakora, ikiwa anaitumia na kusema:
Askofu. Awabariki Mungu mwenyezi,
Baba +, na Mwana +, na Roho Mtakatifu +.

W. Amina.
---------

K. Misa imekwisha: sasa mnatumwa kuiishi Injili.

Au:
K.
Nendeni, mkaitangaze Injili ya Bwana.

Au:
K.
Nendeni na amani, mkimtukuza Bwana kwa maisha yenu.

Au:
K.
Nendeni na amani.
W. Tumshukuru Mungu.

-----------
Pasaka
K. Nendeni na amani, Aleluya, aleluya.
W. Tumshukuru Mungu, Aleluya, aleluya.

Hatimaye kuhani anatoa heshima kwa altare kama kawaida, kama mwanzo wa Misa. Halafu anaiinamia sana pamoja na wahudumu, na anaondoka. Endapo baada ya Misa inafuata ibada nyingine ya kiliturujia, ibada ya kuaga inaachwa.

BARAKA KUU

Baraka hizi zaweza kutumiwa, kwa hiari ya kuhani, mwishoni mwa adhimisho la Misa, au la liturujia ya Neno, au la Ofisyo, au la Sakramenti.

I. Katika maadhimisho ya vipindi maalumu.
1. Majilio
K. Mungu mwenyezi na mwenye huruma apende kuwatakasa kwa uangavu wa ujio wa Mwanae pekee. Nanyi mlioiweka imani yenu katika ujio wake wa kwanza na kungojea kwa matumaini ule wa pili, awajaze utajiri wa baraka zake.
W. Amina.
K. Katika maisha ya sasa hapa duniani Yeye awafanye imara katika imani, wafurahivu katika matumaini na wenye juhudi katika upendo.
W. Amina.
K. Ninyi mnaofurahia sasa kwa moyo wa ibada ujio wa Mkombozi wetu katika mwili, mjaliwe thawabu za uzima wa milele atakapokuja tena katika utukufu wake.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

2. Noeli
K. Mungu mwenye wema usio na mwisho, ambaye kwa njia ya Mwanae aliyejifanya mwanadamu amelifukuza giza ulimwenguni, na kwa kuzaliwa kwake katika utukufu ameiangaza siku hii takatifu sana, apende kuwaondolea gia la upotovu na kuiangaza mioyo yenu kwa nuru ya fadhila.
W. Amina.
K. Mungu aliyemtuma Malaika awapashe wachungaji habari ya furaha kubwa ya kuzaliwa kwa Mwokozi, apende kuijaza mioyo yenu furaha yake, na kuwafanya wajumbe wa Injili yake.
W. Amina.
K. Mungu, kwa njia ya umwilisho wa Mwanae, aliunganisha mambo ya mbinguni na yale ya duniani. Apende kuwajalia nyinyi amani yake na mapenzi mema na kuwashirikisha katika maisha ya Kanisa la mbinguni.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

3. Mwanzoni mwa mwaka
K. Mungu aliye chemchemi na asili ya baraka zote, apende kuwapa neema, awamiminie wingi wa baraka zake, awahifadhi salama na awakinge na madhara yote kwa mwaka mzima.
W. Amina.
K. Awalinde katika ukamilifu wa imani, awajalie ustahimilivu katika matumaini, na udumifu katika upendo mkiwa na saburi takatifu hadi mwisho.
W. Amina.
K. Azipange siku zenu na matendo yenu katika amani yake, ayasikilize maombi yenu kila wakati na popote mlipo, na kuwafikisha kwa furaha katika uzima wa milele.
W. Amina.
K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

4. Epifania ya Bwana
K. Mungu aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu, apende kuwamiminia kwa hisani baraka yake na kuimarisha mioyo yenu katika imani, matumaini na mapendo.
W. Amina.
K. Kwa vile ninyi mnamfuata kwa imani Kristo, ambaye leo amejidhihirisha ulimwenguni kama nuru ing'aayo gizani, awafanye ninyi pia kuwa nuru kwa ndugu zenu.
W. Amina.
K. Baada ya kumaliza maisha yenu hapa duniani, awajalie kumfikia Yeye, ambaye mamajusi walimwona kwa furaha kuu, baada ya kumtafuta wakiongozwa na nyota, Yeye aliye mwanga kutoka kwa mwanga, Kristo Bwana wetu.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

5. Mateso ya Bwana
K. Mungu, Baba wa rehema, ambaye amewapeni mfano wa mapendo kwa mateso ya Mwanae pekee, awajalie ili, kwa kumtumikia Mungu na watu, mpokee zawadi isiyo na kifani ya baraka yake.
W. Amina.
K. Ninyi mnaoamini kwamba kwa kifo chake, amewaepusha na kifo cha milele, mjaliwe zawadi ya uzima wa milele.
W. Amina.
K. Kwa vile mnafuata mfano wa unyenyekevu wake, mjaliwe kushiriki ufufuko wake.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

6. Kipindi cha Pasaka
K. Mungu aliyependa kuwajalia mema ya ukombozi na kuwafanya wana kwa ufufuko wa Mwanae pekee, awajalie mfurahie kwa pamoja baraka yake.
W. Amina.
K. Naye aliyewajalia zawadi ya uhuru wa kudumu, awafanye washiriki wa urithi wa uzima wa milele kwa kazi yake ya ukombozi.
W. Amina.
K. Nanyi mliofufuka katika Ubatizo kwa njia ya imani mstahili kuunganishwa naye katika makao ya mbinguni, kwa kuishi kiadilifu hapa duniani.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

7. Kupaa Bwana
K. Mungu mwenyezi, ambaye siku hii ya leo Mwanae pekee alizipenya mbingu za juu na kuwafungulia njia ya kupaa aliko yeye, awape baraka zake.
W. Amina.
K. Kama Kristo alivyojidhihirisha wazi kwa wanafunzi wake baada ya ufufuko wake, vivyo hivyo atakapokuja kama hakimu, ajidhihirishe kwenu akiwa radhi nanyi kwa milele yote.
W. Amina.
K. Nanyi mnaosadiki kwamba ameketi na Baba katika utukufu wake, mpate kung'amua kwa furaha ukweli wa ahadi yake ya kukaa nanyi hadi mwisho wa nyakati.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

8. Roho Mtakatifu
K. Mungu Baba wa mianga, aliyependa kuangaza akili ya wanafunzi kwa kuwamiminia Roho Mtakatifu Mfariji, awajalieni kufurahia baraka yake, na kujaa daima mapaji ya huyo Roho.
W. Amina.
K. Moto ule wa ajabu, ulioonekana juu ya wanafunzi, uitakase mioyo yenu na kila uovu, na kuifanya iangaze kwa kuimiminia nuru yake.
W. Amina.
K. Na Mungu aliyependa kuunganisha lugha mbalimbali katika ungamo la imani moja, awadumishe ninyi katika imani hiyo; na, kwa kuamini, awajalie kumwona Yeye mnayemtumaini.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

9. Kipindi cha mwaka I
K. Bwana awabariki, na kuwalinda.
W. Amina.
K. Awaangazie nuru ya uso wake, na kuwafadhili.
W. Amina.
K. Awainulie uso wake, na kuwapa amani yake.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

10. Kipindi cha mwaka II
K. Amani ya Mungu ipitayo akili zote iwahifadhi mioyo yenu na nia zenu, katika kumjua na kumpenda Mungu na Mwanae, Bwana wetu Yesu Kristo.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

11. Kipindi cha mwaka III
K. Mungu Mwenyezi awabariki kwa wema wake, na kuwamiminia hekima yake iletayo wokovu.
W. Amina.
K. Na awalishe siku zote kwa mafundisho ya imani, na kuwadumisha katika matendo matakatifu.
W. Amina.
K. Na aelekeze hatua zenu kwake, na kuwaonesha njia ya amani na mapendo.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

12. Kipindi cha mwaka IV
K. Mungu wa faraja yote azipange siku zenu katika amani yake, na awajalie mapaji ya baraka yake.
W. Amina.
K. Awaepushe daima na mahangaiko yote, kuithibitisha mioyo yenu katika upendo wake.
W. Amina.
K. Na awajaze na mapaji ya imani, matumaini na mapendo, ili mpate kuishi maisha haya mkiwa na juhudi katika kazi, na mfike kwa furaha katika uzima wa milele.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

13. Kipindi cha mwaka V
K. Mwenyezi Mungu awakinge daima na maafa yote, na kwa wema wake awashushie mapaji ya baraka yake.
W. Amina.
K. Aifanye mioyo yenu kuwa sikivu kwa maneno yake, ipate kujazwa furaha isiyo na mwisho.
W. Amina.
K. Na kwa kuelewa yaliyo mema na mazuri, daima mwende mbio katika njia ya amri za Mungu, mpate kufanywa warithi pamoja na wateule wa mbinguni.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

14. Kipindi cha mwaka VI
K. Mungu awabariki na kila baraka ya mbinguni, awafanye daima watakatifu na safi machoni pake, awamiminie kwa wingi utajiri wa utukufu wake, na kuwaelimisha kwa maneno ya kweli; awafundishe katika Injili ya wokovu, na daima awatajirishe akiwajalia mapendo ya kidugu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

II. Katika maadhimisho ya Watakatifu
15. Bikira Maria mtakatifu
K. Mungu aliyependa kwa wema wake mkuu kuwakomboa wanadamu, kwa kuzaliwa kwake Mwanae na Bikira Maria Mtakatifu, apende kuwastawisha kwa baraka yake.
W. Amina.
K. Mjaliwe kutambua daima na popote ulinzi wake yeye, ambaye kwa kupitia kwake mmestahili kumpokea muumba wa uzima.
W. Amina.
K. Ninyi mliokusanyika leo kwa moyo wa ibada, mjaliwe kurudi mkiwa na mapaji ya furaha za kiroho na tuzo za mbinguni.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

16. Watakatifu Petro na Paulo
K. Awabariki Mungu mwenyezi, aliyewaimarisha kwa maungamo yaletayo wokovu ya Mtakatifu Petro, na kwa hayo amewaweka juu ya mwamba thabiti wa imani ya Kanisa.
W. Amina.
K. Yeye aliyewaelekeza kwa mahubiri na juhudi ya Mtakatifu Paulo, apende kuwafunza daima kwa mfano wake, mpate kuwaleta ndugu kwa Kristo.
W. Amina.
K. Kwa funguo za Mtakatifu Petro na maneno ya Mtakatifu Paulo, na kwa msaada wa jitihada ya maombezi yao wote wawili, Mungu awaongoze katika makao yale, ambayo Petro aliyafikia kwa njia ya msalaba, na Paulo kwa njia ya upanga.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

17. Mitume
K. Mungu aliyewajalia ninyi kusimama imara juu ya misingi ya Mitume, awe radhi kuwabariki kwa maombezi na mastahili matukufu ya Mitume watakatifu J. na J. (Mtume mtakatifu J.).
W. Amina.
K. Yeye, aliyewajalia ninyi mafundisho na mifano ya Mitume, awafanye mashahidi wa ukweli kwa watu wote, chini ya ulinzi wao.
W. Amina.
K. Kwa maombezi ya Mitume, mjaliwe kuufikia urithi wa makao ya milele, ninyi mliothibitika katika imani kwa njia ya mafundisho yao.
K. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

18. Watakatifu wote
K. Mungu aliye utukufu na furaha ya watakatifu, aliyewaimarisha ninyi kwa maombezi yao bora, awabariki na baraka isiyo na mwisho.
W. Amina.
K. Ninyi mliookolewa na maovu yaliopo sasa kwa maombezi yao, na kuongozwa na mfano wa maisha yao matakatifu, mjaliwe daima kumtumikia Mungu na jirani.
W. Amina.
K. Kanisa takatifu lafurahia kwamba wanawe wanaunganika katika amani ya kudumu na wateule mbinguni. Nanyi mjaliwe kumiliki pamoja na hao wote furaha za makao ya mbinguni.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

III. Baraka nyinginezo
19. Katika kutabaruku kanisa
K. Mungu, Bwana wa mbingu na dunia, aliyewakusanya ninyi leo ili kutabaruku kanisa hili, awajaze baraka za mbinguni.
W. Amina.
K. Yeye aliyependa waliotawanyika wanawe wote wakusanywe pamoja katika Mwanae, awajalie ninyi muwe hekalu lake, na makao ya Roho Mtakatifu.
W. Amina.
K. Nanyi mliotakaswa kwelikweli, Mungu akae ndani yenu, na mpewe urithi wa heri ya milele pamoja na watakatifu wote.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.

----------

20. Katika adhimisho kwa ajili ya marehemu
K. Mungu wa faraja yote awabariki, Yeye ambaye kwa wema wake usio na kifani alimwumba binadamu, na kwa ufufuko wa Mwanae Pekee, amewapa waamini tumaini la kufufuka.
W. Amina.
K. Na sisi tulio hai, Mungu atujalie msamaha wa dhambi; na marehemu wote awajalie mahali pa mwanga na amani.
W. Amina.
K. Sisi sote tunaosadiki kwamba Kristo alifufuka kweli katika wafu, tujaliwe kuishi kwa furaha pamoja naye bila mwisho.
W. Amina.

K. Na baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba, + na Mwana, na Roho Mtakatifu iwashukie na kukaa nanyi daima.
W. Amina.
----------

Hitimisho
K. Nendeni, mkaitangaze Injili ya Bwana.

Au:
K.
Nendeni na amani, mkimtukuza Bwana kwa maisha yenu.

Au:
K.
Nendeni na amani.
W. Tumshukuru Mungu.

-----------
Pasaka
K. Nendeni na amani, Aleluya, aleluya.
W. Tumshukuru Mungu, Aleluya, aleluya.