MARIA MAMA WA MUNGU
SALA ZA MCHANA
chagua SALA YA ADHUHURI
chagua SALA KABLA YA ADHUHURI
Kwa SALA BAADA YA ADHUHURI: endelea hapo chini
BAADA YA ADHUHURI
K. Ee Mungu, uje kutusaidia.
W. Ee Bwana, utusaidie hima.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.
Amina. Aleluya
UTENZI
E Bwana Mbarikiwa
Mungu Muumbaji wetu,
Vitu vyote hutakaswa
Katika Wewe, E Mungu,
Wewe waviimarisha
Hata milele vidumu.
Wenye heri, e mkono
Mtakatifu wa Mungu,
Ndiwe watakatifuza
Vitu vyote, vyote vitu,
Na upya unavitia
Wavipamba vyasitawi.
Ewe fahari tukufu,
Enzi yake Bwana Mungu,
Ndani mwako wachukua
Vyote unavyovijaza;.
Na yote yanafanyika.
Kadiri unavyotaka.
Usifiwe, utukuzwe
Utatu Mtakatifu,
Ujuaye kwa hakika
Na makini zako njia;
Wewe ndiwe nuru kuu.
Milele inayodumu.
ANT.: Macho yangu yameuona wokovu uliouandaa machoni pa watu wote.
Zab.126 Kuomba nguvu mpya
Mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu (2Kor.1:7)
Mungu alipoturudisha tena Sion,*
tulikuwa kama wanaoota ndoto!
Hapo tuliangua kicheko;*
tulishangilia kwa furaha.
Nao watu wa mataifa mengine walisema,*
"Mungu amewatendea mambo makubwa!"
Kweli Mungu alitutendea maajabu,*
tulifurahi kweli kweli!
Ee Mungu, urekebishe tena hali yetu,/
kama mvua inavyotiririsha maji*
katika mabonde makavu.
Wanaopanda kwa machozi*
watavuna kwa shangwe.
Wanaokwenda kupanda mbegu huku wakilia,*
watarudi kwa furaha huku wakichukua mavuno.
Atukuzwe Baba na Mwana*
na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo na sasa na siku zote*
na milele. Amina
Zab.127 Bila Mungu kazi ya binadamu haifai
Ninyi ni jengo lake Mungu (1Kor.3:9)
Mungu asipoijenga nyumba,*.
waijengao wanajisumbua bure.
Mungu asipoulinda mji,*
waulindao wanakesha bure.
Mnaamka mapema asubuhi na kuchelewa kulala usiku,/
mkihangaika na kutoka jasho kupata chakula chenu.*
Kwa nini mnajihangaisha hivyo?
Kama mnampenda Mungu*
atawajalieni yote mngali usingizini!
Watoto ni zawadi itokayo kwa Mungu;*
watoto ni tuzo lake kwetu sisi.
Watoto unaowapata ukiwa kijana,*
ni kama mishale mikononi mwa askari.
Heri mtu aliye na mishale hiyo kwa wingi.*
Hatashindwa akutanapo na adui mahakamani.
Atukuzwe Baba na Mwana*
na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo na sasa na siku zote*
na milele. Amina
Zab.128 Tuzo kwa jamaa imchayo Mungu
'Bwana akubariki kutoka Sion', yaani kutoka Kanisa lake (Arnobius)
Heri wote wamchao Mungu,*
Wanaoishi kufuatana na amri zake.
Kazi zako zitakupatia mahitaji yako,*
utaona furaha na kufanikiwa.
Mke wako atakuwa kama mzabibu*
wenye matunda mengi nyumbani mwako;
watoto wako watakuwa kama machipukizi*
ya mizeituni kuizunguka meza yako.
Naam, ndivyo atakavyobarikiwa*
mtu amchaye Mungu.
Mungu akubariki toka Sion!*
Uione fanaka ya Yerusalemu,
siku zote za maisha yako.*
Uishi na hata uwaone wajukuu wako!
Atukuzwe Baba na Mwana*
na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo na sasa na siku zote*
na milele. Amina
Ant.: Macho yangu yameuona wokovu uliouandaa machoni pa watu wote.
SOMO: Bar.5:3-4
Mungu ataidhihirisha nuru yako duniani mwote, na jina lako litaitwa na Mungu daima, Amani ya
haki, na Utukufu wa utauwa.
K. Rehema na uaminifu vimekutana, aleluya.
W. Haki na amani vimekumbatiana, aleluya.
SALA:
Tuombe: Mungu, Baba yetu, kwa kuwa umewapa wanadamu mwokozi kwa njia ya Maria mwenye heri,
bikira na mama, utujalie tuweze kuhisi nguvu ya maombezi yake wakati anapotuombea kwa Yesu
Kristo, Mwanao, chanzo cha uzima, anayeishi na kutawala daima na milele.
W. Amina.
K. Tumtukuze Bwana.
(W.) tumshukuru Mungu.