JAN.10 au ALHAMISI BAADA YA EPIFANIA
MASOMO
Somo: 1 1Yoh.4:19-5:4
Wapenzi: Sisi twampenda Mungu kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia
ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba
yeye ampendaye Mungu, ampende ndugu yake. Kila mtu aaminiye kwamba Yesu Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu
ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twapenda watoto wa Mungu,
tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku
ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo Imani yetu.
Wimbo wa Katikati Zab.72:1-2, 14-15 (K)11
1. Ee Mungu, mpe mfalme hukumu yako,
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
(K) Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
2. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu,
Na damu yao ina thamani machoni pake.
Na wamwombee daima;
Na kumbariki mchana kutwa. (K)
3. Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa yote na wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri. (K)
SHANGILIO: Lk.7:16
Aleluya, aleluya,
Nabii mkuu ametokea kwetu; na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya
INJILI: Lk.4:14-22
Siku ile, Yesu alirudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na
siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii
Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena,
kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi;
na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni
mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
--------------
--------------
MAOMBI
Wapendwa, hatuwezi kumpenda Mungu ambaye
hatumwoni, kama hatuwezi kuwapenda ndugu zetu
ambao tunawaona. Tumwombe Mungu ili tupate
kuushinda ulimwengu:-
Kiitikio: Twakuomba utusikie.
1. Umjalie kila mbatizwa kuutambua na kuutekeleza
wajibu, wa kuwa mhubiri wa Habari Njema kwa jirani
zake.
2. Utuongezee bidii ya kuzishika amri zako, kama alama
ya kukupenda wewe.
3. Utuzidishie hamu ya kujisomea maandiko matakatifu
kila siku na kuutafakari upendo wako kwetu.
4. Marehemu wetu washirikishwe utukufu wako huko
mbinguni.
Tunayaomba hayo ili, Roho wako Mtakatifu tuliyempokea,
atuongoze katika kushinda kuushindako ulimwengu. Kwa
njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.