ALHAMISI JUMA 1 MAJILIO
MASOMO
SOMO 1: Isa.26:1-6
Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; ataamuru wokovu kuwa kuta
na mamboma. Wekeni wazi malango yake, taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie. Utamlinda yeye ambaye
moyo wake umekutegemea katika Amani kamilifu, kwa kuwa tunakutumaini. Mtumainini Bwana sikuzote, maana
Bwana Yehova ni mwamba wa milele. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha
hata nchi, auleta hata mavumbini. Mungu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao
walio wahitaji.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.118:1,8-9,19-21,25-27a
1. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
Kwa maana fadhili zake ni za milele,
Ni heri kumkimbilia Bwana,
Kuliko kuwatumainia wanadamu,
Ni heri kumkimbilia Bwana
Kuliko kuwatumainia wakuu. (K)
(K) Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
2. Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru Bwana.
Lango hili ni la Bwana,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu. (K)
3. Ee Bwana, utuokoe, twakusihi,
Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana,
Tumewabarikia toka nyumbani mwa Bwana.
Bwana ndiye aliye Mungu,
Naye ndiye aliyetupa nuru. (K)
Shangilio: Isa.55:6
Aleluya, aleluya,
Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni maadamu yu karibu.
Aleluya.
INJILI: Mt.7:21,24-27
Siku ile, Yesu akawaambia wafuasi wake: Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme
wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Basi kila asikiaye hayo maneno
yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, mvua ikanyesha,
mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya
mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba
juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo
anguko lake likawa kubwa.
--------------
--------------
MAOMBI
Kwa kuwa sisi tumeandaliwa mji ulio na nguvu na Bwana ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma, kwa matumaini
tunasali:
Kiitikio: Bwana utusikie, Bwana utusikilize.
1. Uwalinde Papa wetu F., Askofu wetu F. na
viongozi wetu wote wa dini na wa serikali na wale wote wanaokutumaini katika amani kamilifu.
2. Utujalie sisi sote kuyaweka wazi malango yako, ili tuwe watu wenye haki, tushike kweli yako na
tukuabudu wewe.
3. Uwashushe wenye kiburi na kuwakweza wanyenyekevu.
4. Utukumbushe kuyatimiza mapenzi yako ili siku ya mwisho tuingie katika ufalme wako wa mbinguni.
Ee Bwana uliyemuumba wa milele, utuonee huruma sisi tulio wanyonge na wahitaji. Utujalie udumifu katika
imani ya Kanisa lako lililojengwa katika msingi imara. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.