KITUBIO

Pima mwenendo wako mbele ya Mungu
- Je, ulipoungama mara ya mwisho uliungama vizuri, ukatimiza malipizi yako?
- Umekuwa mtu mwenye ibada kwa Mungu, au ulipurukusha sala zako kwa namna yoyote?
- Umekuwa na adabu njema kwa mambo ya dini; kwa mfano hukutumia jina takatifu la Mungu ovyo ovyo?
- Je, uliadhimisha Dominika kwa kushiriki Misa takatifu? Au labda umekosa kufika kwa kosa lako mwenyewe; au kuchelewa?
- Na wakati ulipokuwa kanisani, je, uliweka moyo wako mbele ya Mungu; au umetumia wakati wako kwa kuwaangalia watu wengine na kuchezacheza?
- Je, ulimwamini na kumtumaini Mungu, anayekuangalia na aliyekupa malaika mlinzi wa kukulinda? Au labda ulikosa uaminifu kwake?
- Umeonesha mbele ya Mungu kwamba wampenda, kwasababu Yeye mwenyewe anakupenda sana? Umevumilia kwa moyo wote masumbuko ya maisha yako? Je, umelipa zaka na michango ya Kanisa?