KITUBIO

Pima matendo yako nafsini mwako mwenyewe.
- Je, mawazo yako yamekuwa mazuri au ya aibu mbele ya Mungu wako? Kumbuka kama mwilio ndio hekalu la Roho Mtakatifu kwa ajili ya neema. Je, umekuwa na heshima kwa mwili wako?
- Je, umejitahidi kuzingatia fadhila ya kiasi katika kula na kunywa?
- Je, una majivuno, kwa kutaka kusifiwa na watu kupita kiasi, na kutaka kuwatawala wengine?