KITUBIO

Kama una ndoa, jipime kama umekaa vizuri katika ndoa yako.
- Umempenda mwenzi wako wa ndoa na umemfurahisha? Umemvumilia au umempiga mwenzio na kumtia uchungu kwa maneno yako?
- Je, umekuwa mtu wa kulewa mara kwa mara, na kutopenda kukaa na familia yako?
- Je, umetumia vibaya mshahara wako?
- Je, umefanya yakupasayo juu ya watoto wako: kuwalea vizuri; kuonesha kwamba wawapenda; kuwapa nguo zahali yao; kuwapatia mafundisho ya dini; kuwakinga wasipotoshwe na watu wabaya; kuwachunga wasitembee na marafiki wabaya; kuwafurahisha mara kwa mara na kuwapendeza ili wapate kusikiliza maonyo na kushika mfano mzuri?