KITUBIO

Pima mwenendo wako mbele ya wenzako.
-Je, umewastahi wazazi wako, wakubwa wako, waalimu n.k.; au umekosa utii na heshima kwao kwa kiburi?
-Umewadanganya kwa maneno ya uongo, kuwahadaa kwa hila, au kuficha ukweli kwa namna nyingine?
- Umewasaidia wazazi na wakubwa wengine kwa jinsi ulivyoweza katika kazi yao; au umependa zaidi kupiga uvivu? Je, umewaacha wazazi wako katika umaskini?
- Je, umeifanya sawasawa kwa bidii ile kazi inayokupasa uifanye, au umetegea na kupewa mshahara bila kustahili?
- Umekuwa mwema kwa watu wengine, mpole, mkarimu, mpendelevu? Au unaelekea kukasirika, kupigana, kutukana, na mambo kama hayo?
- Umefanya bidii ya kuwafundisha watu wengine matendo mema; au labda umewasaidia kutenda dhambi, au kuwapa nafasi ya dhambi?
- Umekuwa mtu wa kugawana chakula chako na wenziwako kwa ukarimu, au labda umekuwa mwenye ulafi auchoyo?
- Umetunza ulimi ili usimsengenye mtu na kumdhuru kwa sifa za jina lake? Je, umeiba kitu chochote, au kuharibu mali ya mtu? Umerudisha na kufidia hasara?