25
Jibu la Bildadi 1 Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu: 2 “Mungu ni mwenye uwezo mkuu, watu wote na wamche. Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni. 3 Nani awezaye kuhesabu majeshi yake? Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake? 4 Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu? Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi? 5 Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha; nyota nazo si safi mbele yake; 6 sembuse mtu ambaye ni mdudu, binadamu ambaye ni buu tu!”