B

Mfalme Ahasuero aamuru Wayahudi wauawe
1 Hii ni nakala ya barua hiyo, “Mfalme mkuu Ahasuero anawatumia barua ifuatayo wakuu wa mikoa yake 127, inayoenea tangu India hadi Ethiopia, pamoja na wakuu walio chini yao:
2 “Baada ya kuwa mtawala wa mataifa mengi na bwana wa dunia nzima, niliamua kuwa maisha ya raia wangu lazima yawe katika amani daima. Nilitaka hilo, si kwa sababu ya majivuno yanayotokana na mamlaka yangu, bali kwa sababu daima nimekuwa nikitenda kwa busara na kuwatawala raia wangu kwa upole. Nilidhamiria kuirudisha amani na kupanga lolote linalowezekana ili kujenga ufalme uliostaarabika wenye usalama wa kusafiri, toka pembe hii hadi pembe nyingine.
3 Nilipowauliza washauri wangu namna ya kufikia lengo hilo, Hamani akatoa uamuzi wake. Yeye anatambuliwa miongoni mwetu kuwa mtu mwenye hekima kubwa. Daima ameonesha waziwazi kuwajibika kwake katika ustawi wa ufalme. Kutokana na uaminifu wake wa kudumu, yeye amepandishwa cheo na kuwa mtu wa pili katika ufalme.
4 Ni hivi majuzi tu, alitueleza juu ya taifa fulani adui ambalo watu wake wameenea kote katika ufalme huu. Taifa hilo linapingana na kila taifa, lina sheria zake na daima linazidharau amri za kifalme. Matokeo ya tabia yao ni kwamba sisi hatuwezi kuleta umoja wa serikali ambao tunautaka kwa moyo.
5 “Tunafahamu kuwa ni watu hawa peke yao walio wapinzani wa kila mtu. Watu hawa ni wapinzani wa serikali yetu na wanafanya maovu mengi ambayo yanahatarisha usalama na uthabiti wa ufalme. Wanafuata desturi za kigeni na sheria zao wenyewe.
6 Kwa hiyo, tunaagiza kuwa watu wanaotajwa katika barua zake Hamani, mtu anayeshikilia nafasi ya pili na ni kama baba katika ufalme huu, watu hao wote, wanawake pamoja na watoto wauawe. Waangamizwe kwa upanga wa adui zao, bila kuwaonea huruma hata kidogo. Agizo hili litekelezwe siku ya kumi na nne ya mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari, mwaka huu.
7 Watu hawa, ambao kwa muda mrefu wamesababisha matatizo mengi, kwa siku moja watakufa kifo cha kikatili na kwenda kuzimu. Halafu wataiacha serikali yetu ikiwa salama salimini na bila matatizo.”

3

14 Taarifa hiyo ilitakiwa ibandikwe hadharani katika kila mkoa, ili kila mtu ajiandae kwa ajili ya siku hiyo.
15 Kwa amri ya mfalme, tangazo hili lilitolewa katika mji mkuu wa Susa, nao matarishi wakalitangaza katika mikoa yote. Mfalme na Hamani walikaa wanastarehe pamoja wakati watu mjini Susa wanafadhaika.

Generic placeholder image