E

Agizo la mfalme kuwatetea Wayahudi
1 Ifuatayo ni nakala ya agizo hilo: “Kutoka kwa mfalme mkuu Ahasuero, kwa wakuu wa mikoa 127, inayoenea tangu India mpaka Ethiopia, na kwa wote walio watiifu kwa serikali yetu. Salamu.
2 “Watu wengi, kwa kadiri wanavyoheshimiwa na kupewa upendeleo mwingi na wakubwa wao, ndivyo wanavyozidi kuwa na kiburi.
3 Si kwamba wanataka kuwadhuru raia wetu tu, bali, wakiwa hawawezi kuvumilia ufanisi wetu, wanakula njama dhidi ya wafadhili wao.
4 Hawana shukrani kwa yale waliyotendewa na watu, ila, wakiwa wamekumbwa na majivuno ya watu wasiojua ni nini wema, wanadhani wataweza hata kukwepa hukumu ya Mungu achukiaye uovu na aonaye vitu vyote.
5 Mara nyingi wale walioko kwenye madaraka wamehusishwa katika umwagaji damu isiyo na hatia na hao rafiki waliopewa mamlaka ya uendeshaji wa shughuli za umma. Na kwa sababu hiyo wamesababisha maafa makubwa ambayo haiwezekani sasa kuyarekebisha.
6 Rafiki hawa, kwa uongo wao na mienendo yao ya udanganyifu, wanatumia nia njema ya watawala wao kwa manufaa yao wenyewe.
7 Mnaweza kujionea wenyewe mifano ya matumizi mabaya ya mamlaka, si tu kutokana na masimulizi ambayo yapo tangu kale hadi sasa, bali hata yale machafuko yaliyotendeka miongoni mwetu hivi karibuni.
8 “Nitajitahidi kuhakikisha kuwa wakati ujao ufalme wangu hautakuwa na misukosuko bali utabaki na amani kwa ajili ya watu wote.
9 Hili litafanyika kwa kubadilisha misimamo kadhaa na kuamua kwa haki kila suala linapoletwa mbele yangu.
10 “Fikirini kwa mfano juu ya Hamani, mwana wa Hamedatha, kutoka Makedonia. Yeye ni mgeni, asiye na damu yoyote ya Wapersi na hana dalili yoyote ya shukrani kwa wema wetu. Sisi tulimkaribisha,
11 naye akafaidi wema wetu na upendo tulio nao kwa watu wote. Na kwa kweli sisi tukamtangaza kama ‘Baba wa ufalme wetu,’ tukampa heshima kubwa kuliko mtu mwingine yeyote, isipokuwa mfalme peke yake.
12 Lakini ufidhuli wake haukujua mipaka akajaribu kuyaondoa maisha yangu na hivyo kupindua ufalme.
13 Kwa njia za kijanja na hila, akaniomba nimwue Mordekai. Mordekai ni mtu aliyeyaokoa maisha yangu na mtu ambaye daima ametuunga mkono. Hamani, hata aliniomba nimwue Esta, malkia wetu asiye na hatia. Na kwa kweli, alitaka kuliangamiza taifa zima la Wayahudi.
14 Lengo lake hasa lilikuwa kutuacha sisi bila ulinzi wowote, halafu watu wa Makedonia wangelikuja na kuchukua ufalme wa Persia.
15 “Lakini tumegundua kuwa Wayahudi, watu ambao Hamani, mtu mwovu aliyelaaniwa, alinitaka kuwafutilia mbali duniani, si wasaliti hata kidogo. Bali wao hutawaliwa na sheria za haki kabisa,
16 na ni watu wake Mungu aliye hai, Mungu Mkuu na mwenye nguvu ambaye ameuongoza na kuufanikisha huu ufalme kwa faida ya wazee wetu na sasa kwa faida yetu.
17 “Kwa hiyo mtakuwa mnatenda jambo jema kabisa ikiwa hamtatekeleza maagizo yaliyotolewa na Hamani katika barua zake,
18 kwa vile yeye ndiye aliyehusika na mambo haya yote na tayari amekwisha tundikwa mtini pamoja na jamaa yake kwenye lango la mji wa Susa. Mungu anayetawala mambo yote amemwadhibu haraka kama alivyostahili.
19 “Kwa hiyo bandikeni nakala ya agizo hili popote hadharani, na kuwaruhusu Wayahudi waishi kulingana na sheria zao.
20 Wapeni msaada wanapojilinda dhidi ya wanaowashambulia siku ile iliyowekwa ili kuwaangamiza, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili.
21 Mungu anayetawala mambo yote, ameibadilisha siku hiyo ya maangamizi iwe siku ya sherehe kwa watu wake aliowachagua.
22 “Siku hiyo itakuwa ni mojawapo ya sikukuu zenu za taifa, nanyi isherehekeeni kwa furaha.
23 Kuanzia sasa, hata wakati ujao, itatukumbusha sisi pamoja na washiriki wenzetu jinsi Mungu anavyolichunga taifa letu la Persia, na kwamba wote wanaopanga maovu dhidi yetu watakumbushwa juu ya maangamizi ya Mungu.
12z Kila mkoa wowote ule au mji wowote usiotii agizo langu hili, utakumbwa na ghadhabu yangu, na kuangamizwa kwa mkuki na kwa moto. Hakuna mwanaadamu yeyote atakayekanyaga huko hata, ndege na wanyama wataukwepa kabisa milele.”

8

13 Nakala za tangazo hili ambalo lilitolewa kama sheria katika kila mkoa zilisambazwa kwa kila mtu katika kila mkoa, ili Wayahudi wajiandae kulipiza kisasi siku hiyo ifikapo.
14 Kwa amri ya mfalme, matarishi waliopanda farasi wenye nguvu waendao kasi, waliondoka mbio. Tangazo hili pia lilitolewa katika mji mkuu, Susa.
15 Mordekai alipotoka ikulu kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi ya kifalme ya rangi ya urujuani na nyeupe, joho la kitani safi la rangi ya zambarau, na taji kubwa ya dhahabu, mji wa Susa ulijaa shangwe na vigelegele. 16Hapo Wayahudi waliona fahari, heshima na furaha, wakajisikia wenye nafuu na ushindi. 17Katika kila mkoa na kila mji, popote pale tangazo hili liliposomwa, Wayahudi walifurahi na kushangilia, wakafanya sherehe na mapumziko; na watu wengine wengi wakajifanya kuwa Wayahudi, maana waliwaogopa sana Wayahudi.
16 Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.
17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.

Generic placeholder image