9

Safari kwenda Rage
1 Baada ya hayo, Tobia alimwita Rafaeli, akamwambia,
2 “Ndugu Azaria, chukua watumishi wanne na ngamia wawili uende mjini Rage, kwa Gabaeli, umpe hati hii yenye sahihi naye atakupa ile fedha. Halafu uje naye kwenye harusi yangu.
3 Wajua kwamba baba yangu anahesabu siku za kurudi kwangu na nikichelewa hata siku moja tu itamtia wasiwasi mkubwa.
4 Sasa wewe mwenyewe waona mambo ambayo Ragueli ameapa kuyafanya, nami nabanwa na kiapo chake!”
5 Basi, Rafaeli akaenda Rage, akalala nyumbani kwa Gabaeli. Rafaeli akampa Gabaeli ile hati yenye sahihi, na akamwarifu kwamba Tobia mwana wa Tobiti alikuwa anaoa na kwamba alimwalika kwenye harusi hiyo. Bila kukawia, Gabaeli akahesabu mifuko ya fedha iliyokuwa imefungwa na kutiwa mhuri, akamkabidhi Rafaeli.
6 Kesho yake, asubuhi na mapema, Rafaeli na Gabaeli walianza safari kwenda kwenye harusi. Walipowasili nyumbani kwa Ragueli, walimkuta Tobia karamuni. Mara Tobia akainuka kumsalimu Gabaeli ambaye alitokwa machozi na kuwatakia baraka kwa maneno haya: “Wewe ni kijana mzuri wa baba mnyofu na mwadilifu katika shughuli zake zote! Bwana Mungu akujalie baraka za mbinguni wewe na mke wako pamoja na wazazi wa mkeo. Atukuzwe Mungu aliyenijalia kuiona sura hai ya binamu yangu Tobiti!”

Generic placeholder image