1

Ukweli wa Mungu waleta uhai
1 Pendeni haki, enyi watawala wa dunia! Jiaminisheni kikamilifu kwa Bwana. na kumtafuta kwa moyo mnyofu.
2 Maana yeye huwajalia wanaojiaminisha kwake wampate; hujionesha kwa wale wanaomtegemea.
3 Fikira potovu huwatenganisha watu mbali na Mungu; watu wakiijaribu nguvu yake, yeye hudhihirisha upumbavu wao.
4 Hekima haiingii kwa mtu mdanganyifu, wala haikai kwa mtu aliye mtumwa wa dhambi.
5 Mtu aliye mtakatifu amejifunza kuepukana na udanganyifu. Mtu huyo huepa kushiriki fikira za kipumbavu; huwa na wasiwasi endapo haki zinavunjwa ovyo.
6 Hekima ana moyo wa huruma; lakini hatamsamehe yeyote anayemkufuru Mungu. Mungu ajua yote: Hisia zetu na fikira zetu; husikia kila neno tusemalo.
7 Roho ya Bwana inaujaza ulimwengu; hiyo inayotegemeza kila kitu pamoja. hujua kila kitu asemacho binadamu.
8 Kila mtu asemaye mabaya dhidi yake hawezi kufichika, na hukumu inapotolewa hataweza kuiepa adhabu.
9 Mawazo ya waovu yatachunguzwa; Bwana atapata ripoti ya maneno yao mabaya na kuwaadhibu kwa sababu ya uovu wao.
10 Bwana ametega sikio lake; anasikia kila kitu. Hakuna mnongono wowote ule ambao utasitirika.
11 Kwa hiyo jihadharini na manunguniko ya bure, epukeni kusema uchongezi. Mungu husikia hata nunguniko la siri kabisa. Asemaye uongo huiangamiza roho yake mwenyewe.
12 Kwa hiyo usijiletee kifo kwa dhambi zako, wala kukaribisha maangamizi kwa matendo yako maovu.
13 Kifo hakikuanzishwa na Mungu; Mungu hafurahii kufa kwa mtu yeyote yule.
14 Mungu aliumba viumbe vyote vipate kuwapo, akavipa nguvu zifaazo za kuendeleza maisha. Ndani ya viumbe hamna sumu ya kuua; Kuzimu haina mamlaka hapa duniani.
15 Mwadilifu ataishi milele!

Fikira potovu huleta kifo
16 Lakini wasiomcha Mungu hukaribisha kifo kwa matendo na maneno yao, hufanya urafiki na kifo na kufanya mkataba pamoja nacho; sasa wanastahili kuwa mateka wake!

Generic placeholder image