9

Wanawake
1 Usimwonee wivu mke umpendaye; utakuwa umemfundisha namna ya kukudhuru.
2 Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa.
3 Usifuatane na mwanamke wa tabia mbaya, la sivyo utanaswa katika mitego yake.
4 Usishirikiane na mwanamke mwanamuziki, la sivyo, utanaswa kwa werevu wake.
5 Usimtazame kijana msichana mzuri; la sivyo, wewe na yeye mtapata adhabu ileile.
6 Usimpe malaya moyo wako, la sivyo utapoteza nchi yako yote.
7 Usipepesepepese macho mitaani mjini, wala kuzururazurura kwenye maeneo yake ya pekee.
8 Usimtazame mwanamke mzuri, usimkodolee macho mwanamke mrembo asiye wako. Maana wengi wameangushwa kwa uzuri wa mwanamke, maana jambo hilo hufanya tamaa kuwaka kama moto.
9 Kamwe usiketi na mke wa mtu, wala kuketi naye kunywa pombe; la sivyo moyo wako utampenda nawe utakosa kujizuia ukaangamia.

Urafiki na wanaume wengine
10 Usimtupe rafiki wa miaka mingi, maana rafiki mpya hatalingana naye. Rafiki mpya ni kama divai mpya; divai ya miaka mingi hunywewa kwa furaha.
11 Usimwonee kijicho mwenye dhambi akifanikiwa, maana hujui mwisho wake utakuwaje.
12 Usifurahie yanayowapendeza wasiomcha Mungu. Kumbuka hawataepa kuadhibiwa hapahapa duniani.
13 Kaa mbali na mtu anayeweza kukuua, nawe hutakuwa na wasiwasi wa kuuawa. Kama ukimkaribia, uwe na tahadhari; la sivyo, utayaangamiza maisha yako. Ujue kuwa unatembea kwenye mtego hatari, na kwamba unatembea kwenye uwanja wa vita.
14 Wafahamu jirani zako kadiri uwezavyo na kuwaomba ushauri watu wenye hekima.
15 Mazungumzo yako yawe na wenye akili, na mazungumzo yako yote yahusu sheria ya Mungu Mkuu.
16 Watu wanyofu wawe wenzako katika kula, majivuno yako yawe katika kumcha Bwana.

Watawala
17 Kazi ya mtu mwenye juhudi itapata sifa; kiongozi wa watu sharti awe hodari katika maneno yake.
18 Mtu aropokaye ni kitisho mjini kwake; mtu wa maneno ya ovyo huchukiwa.

Generic placeholder image