110

Kutawazwa kwa mfalme mteule
(Zaburi ya Daudi)
1 Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu: “Keti upande wangu wa kulia, hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
2 Mwenyezi-Mungu ataeneza enzi yako kutoka Siyoni; utatawala juu ya maadui zako wote.
3 Watu wako watakujia kwa hiari, siku utakapokwenda kuwapiga maadui. Juu ya milima mitakatifu watakujia vijana wako, kama umande unaotokeza alfajiri mapema.
4 Mwenyezi-Mungu amekuapia wala hatabadili nia yake: “Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”
5 Bwana yuko upande wako wa kulia; atawaponda wafalme atakapokasirika.
6 Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi; atawaponda viongozi kila mahali duniani.
7 Mfalme atakunywa maji ya kijito njiani; naye atainua kichwa juu kwa ushindi.

Generic placeholder image