150

Zaburi ya kumsifu Mungu
1 Msifuni Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mungu katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu zake kuu.
2 Msifuni kwa sababu ya matendo yake makuu; msifuni kwa ajili ya utukufu wake mkuu.
3 Msifuni kwa mlio wa tarumbeta; msifuni kwa zeze na kinubi!
4 Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa filimbi na banjo!
5 Msifuni kwa kupiga matoazi. Msifuni kwa matoazi ya sauti kubwa.
6 Kila kiumbe hai kimsifu Mwenyezi-Mungu! Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Generic placeholder image