123

Kuomba huruma
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Nakutazamia kwa hamu, ee Mwenyezi-Mungu, nakuangalia wewe utawalaye huko juu mbinguni!
2 Kama watumishi wamtegemeavyo bwana wao, kama mjakazi amtegemeavyo bibi yake, ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mpaka hapo utakapotuonea huruma.
3 Utuhurumie, ee Mwenyezi-Mungu, utuhurumie, maana tumedharauliwa kupita kiasi.
4 Tumeshiba muda mrefu dharau za matajiri, tumepuuzwa mno na wenye kiburi.

Generic placeholder image