53

Mtu asiyemcha Mungu(taz Zaburi ya 14)
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi)
1 Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema.
2 Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.
3 Lakini wote wamekosa, wote wamepotoka pamoja, hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja.
4 “Je, hao watendao maovu hawana akili? Wanawatafuna watu wangu kama mikate; wala hawanijali mimi Mungu!”
5 Hapo watashikwa na hofu kubwa, hofu ambayo hawajapata kuiona; maana Mungu ataitawanya mifupa ya adui, hao wataaibika maana Mungu amewakataa.
6 Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni! Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake, wazawa wa Yakobo watashangilia; Waisraeli watafurahi.

Generic placeholder image