13

Kuomba msaada
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1 Mpaka lini ee Mwenyezi-Mungu, utanisahau? Je, utanisahau mpaka milele? Mpaka lini utanificha uso wako?
2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu?
3 Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo.
4 Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!” Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu.
5 Lakini mimi nazitumainia fadhili zako; moyo wangu na ufurahie wokovu wako.
6 Nitakuimbia wewe, ee Mwenyezi-Mungu, kwa ukarimu mwingi ulionitendea!

Generic placeholder image