125

Usalama wa watu wa Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.
2 Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima, ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake, tangu sasa na hata milele.
3 Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu; wasije waadilifu nao wakafanya maovu.
4 Ee Mwenyezi-Mungu, uwe mwema kwa watu wema, kwa wale wanaozitii amri zako.
5 Lakini wanaogeuka na kufuata njia zao mbaya uwakumbe pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli!

Generic placeholder image