122

Sifa za Yerusalemu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 Nilifurahi waliponiambia: “Twende nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.”
2 Sasa tuko tumesimama, kwenye malango yako, ee Yerusalemu!
3 Yerusalemu, mji uliojengwa, ili jumuiya ikutane humo.
4 Humo ndimo makabila yanamofika, naam, makabila ya Israeli, kumshukuru Mwenyezi-Mungu kama alivyoagiza.
5 Humo mmewekwa mahakama ya hukumu ya haki, mahakama ya ukoo wa kifalme wa Daudi.
6 Uombeeni Yerusalemu amani: “Wote wakupendao na wafanikiwe!
7 Ndani ya kuta zako kuwe na amani, majumbani mwako kuweko usalama!”
8 Kwa ajili ya jamaa na ndugu zangu, ee Yerusalemu, nakutakia amani!
9 Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ninakuombea upate fanaka!

Generic placeholder image