120

Kuomba msaada
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu, naye akanijibu.
2 Uniokoe ee Mwenyezi-Mungu, na watu wadanganyifu na waongo.
3 Enyi watu wadanganyifu, mtapewa kitu gani? Mtaadhibiwa namna gani?
4 Kwa mishale mikali ya askari, kwa makaa ya moto mkali!
5 Ole wangu kwamba naishi kama mgeni huko Mesheki; naishi kama mgeni katika mahema ya Kedari.
6 Nimeishi muda mrefu mno kati ya watu wanaochukia amani!
7 Wakati ninaposema nataka amani, wao wanataka tu vita.

Generic placeholder image