75

Mungu hakimu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo ā€œUsiharibuā€. Zaburi ya Asafu. Wimbo)
1 Tunakushukuru, ee Mungu, tunakushukuru! Tunatangaza ukuu wa jina lako na kusimulia juu ya matendo yako makuu.
2 Mungu asema: ā€œMimi nimeweka wakati maalumu! Wakati huo nitahukumu kwa haki.
3 Nchi ikitetemeka na vyote vilivyomo, mimi ndiye ninayeitegemeza misingi yake.
4 Nawaambia wenye kiburi: ā€˜Acheni kujigambaā€™; na waovu: ā€˜Msioteshe pembe za kiburi!
5 Msijione kuwa watu wa maana sana, wala kusema maneno ya majivuno.ā€™ā€
6 Hukumu haitoki mashariki au magharibi; wala haitoki nyikani au mlimani.
7 Mungu mwenyewe ndiye hakimu; humshusha mmoja na kumkweza mwingine.
8 Mwenyezi-Mungu, anashika kikombe mkononi, kimejaa divai kali ya hasira yake; anaimimina na waovu wote wanainywa; naam, wanainywa mpaka tone la mwisho.
9 Lakini mimi nitafurahi milele, nitamwimbia sifa Mungu wa Yakobo.
10 Atavunja nguvu zote za watu waovu; lakini nguvu za waadilifu ataziimarisha.

Generic placeholder image