124

Mungu kinga yetu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 “Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu Semeni nyote mlio katika Israeli:
2 “Kama Mwenyezi-Mungu asingalikuwa upande wetu, wakati ule tuliposhambuliwa na maadui,
3 hakika tungalimezwa tukiwa hai, wakati hasira zao zilipotuwakia.
4 Tungalikumbwa na gharika, tungalifunikwa na mto wa maji,
5 mkondo wa maji ungalituchukua!”
6 Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, ambaye hakutuacha makuchani mwao.
7 Tumeponyoka kama ndege mtegoni; mtego umeteguliwa, nasi tukaokoka.
8 Msaada wetu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.

Generic placeholder image