129

Sala dhidi ya maadui wa Israeli
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu Kila mtu katika Israeli na aseme:
2 “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda.
3 Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu, wakafanya kama mkulima anayelima shamba.
4 Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.”
5 Na waaibishwe na kurudishwa nyuma, wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni.
6 Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua,
7 hakuna anayejishughulisha kuzikusanya, wala kuzichukua kama matita.
8 Hakuna apitaye karibu atakayewaambia: “Mwenyezi-Mungu awabariki! Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”

Generic placeholder image