15

Rafiki ya Mungu
(Zaburi ya Daudi)
1 Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu?
2 Ni mtu aishiye bila lawama, atendaye daima yaliyo mema, asemaye ukweli kutoka moyoni;
3 ni mtu asiyesengenya watu, asiyemtendea uovu rafiki yake, wala kumfitini jirani yake;
4 ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu; ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara;
5 asiyekopesha fedha yake kwa riba, wala kupokea rushwa kumdhulumu asiye na hatia. Mtu atendaye hayo, kamwe hatatikisika.

Generic placeholder image