98

Mungu mtawala wa dunia yote
1 Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu! Mkono wake hodari, mkono wake mtakatifu umempatia ushindi.
2 Mwenyezi-Mungu ameonesha ushindi wake; ameyadhihirishia mataifa uwezo wake wa kuokoa.
3 Amekumbuka fadhili na uaminifu wake kwa Waisraeli. Pande zote za dunia zimeuona ushindi wa Mungu wetu.
4 Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele.
5 Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa shangwe, msifuni kwa sauti tamu za zeze.
6 Mpigieni vigelegele Mwenyezi-Mungu mfalme wetu, mshangilieni kwa tarumbeta na sauti ya baragumu.
7 Bahari na ivume na vyote vilivyomo; dunia na wote waishio ndani yake.
8 Enyi mito pigeni makofi; enyi vilima imbeni pamoja kwa shangwe.
9 Shangilieni mbele ya Mwenyezi-Mungu, maana anakuja kutawala dunia. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, atawatawala watu kwa uadilifu.

Generic placeholder image