130

Kuomba msaada
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Toka upeo wa unyonge wangu, nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu.
2 Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu.
3 Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana, angeweza kusalimika?
4 Lakini kwako twapata msamaha, ili sisi tukuheshimu.
5 Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake.
6 Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko; kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.
7 Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu, maana kwake Mwenyezi-Mungu kuna fadhili, kwake kuna nguvu kubwa ya kutukomboa.
8 Yeye atawakomboa watu wa Israeli kutoka katika maovu yao yote.

Generic placeholder image