131

Kumtumainia Mungu kwa utulivu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi; mimi si mtu wa majivuno. Sijishughulishi na mambo makuu, au yaliyo ya ajabu mno kwangu.
2 Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani, kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake; ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu.
3 Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu, tangu sasa na hata milele.

Generic placeholder image