113

Sifa kwa Mungu mtukufu
1 Msifuni Mwenyezi-Mungu! Enyi watumishi wa Mwenyezi-Mungu, lisifuni jina lake!
2 Jina lake litukuzwe, sasa na hata milele.
3 Kutoka mashariki na hata magharibi, litukuzwe jina la Mwenyezi-Mungu!
4 Mwenyezi-Mungu atawala juu ya mataifa yote, utukufu wake wafika juu ya mbingu.
5 Nani aliye kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu? Yeye ameketi juu kabisa;
6 lakini anatazama chini, azione mbingu na dunia.
7 Humwinua fukara kutoka mavumbini; humnyanyua maskini kutoka unyonge wake,
8 na kumweka pamoja na wakuu; pamoja na wakuu wa watu wake.
9 Humjalia mwanamke tasa furaha nyumbani kwake; humfurahisha kwa kumjalia watoto. Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Generic placeholder image