137

Ombolezo ugenini
1 Kando ya mito ya Babuloni, tulikaa, tukawa tunalia tulipokumbuka Siyoni.
2 Katika miti ya nchi ile, tulitundika zeze zetu.
3 Waliotuteka walitutaka tuwaimbie; watesi wetu walitutaka tuwafurahishe: “Tuimbieni mojawapo ya nyimbo za Siyoni!”
4 Twawezaje kuimba wimbo wa Mwenyezi-Mungu katika nchi ya kigeni?
5 Ee Yerusalemu, kama nikikusahau, mkono wangu wa kulia na ukauke!
6 Ulimi wangu na uwe mzito, kama nisipokukumbuka wewe, ee Yerusalemu; naam, nisipokuthamini kuliko furaha yangu kubwa!
7 Ee Mwenyezi-Mungu, usisahau waliyotenda Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipotekwa; kumbuka waliyosema: “Bomoeni mji wa Yerusalemu! Ngoeni hata na misingi yake!”
8 Ee Babuloni, utaangamizwa! Heri yule atakayekulipiza mabaya uliyotutenda!
9 Heri yule atakayewatwaa watoto wako na kuwapondaponda mwambani!

Generic placeholder image