3

Kuomba msaada asubuhi
(Zaburi ya Daudi alipomkimbia Absalomu)
1 Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu, ni wengi mno hao wanaonishambulia.
2 Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.”
3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu.
4 Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.
5 Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza.
6 Sitayaogopa maelfu ya watu, wanaonizingira kila upande.
7 Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru.
8 Mwenyezi-Mungu ndiwe uokoaye; uwape baraka watu wako.

Generic placeholder image