121

Mungu kinga yetu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.
3 Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii.
4 Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali.
5 Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga.
6 Mchana jua halitakuumiza, wala mwezi wakati wa usiku.
7 Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako.
8 Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.

Generic placeholder image