23

Mungu mchungaji wangu
(Zaburi ya Daudi)
1 Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
2 Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu,
3 na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani yake.
4 Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.
5 Umeniandalia karamu mbele ya maadui zangu; umenipaka mafuta kichwani pangu; kikombe changu umekijaza mpaka kufurika.
6 Kweli wema wako na fadhili zako zitakuwa pamoja nami, siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu milele.

Generic placeholder image