67

Wimbo wa shukrani
(Kwa Mwimbishaji: Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo)
1 Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema;
2 dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa.
3 Watu wote wakutukuze, ee Mungu; watu wote na wakusifu!
4 Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana wawahukumu watu kwa haki, na kuyaongoza mataifa duniani.
5 Watu wote wakutukuze, ee Mungu; watu wote na wakusifu!
6 Nchi imetoa mazao yake; Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
7 Mungu aendelee kutubariki. Watu wote duniani na wamche.

Generic placeholder image