87

Sifa ya Yerusalemu
(Zaburi ya Wakorahi. Wimbo)
1 Mungu amejenga mji wake juu ya mlima wake mtakatifu.
2 Mwenyezi-Mungu anaupenda mji wa Siyoni, kuliko makao mengine ya Yakobo.
3 Mambo ya fahari yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
4 “Miongoni mwa wale wanijuao mimi, wapo watu wa Misri na Babuloni. Kadhalika Filistia, Tiro na Kushi, wote walizaliwa kwako!”
5 Na kuhusu Siyoni itasemwa: “Siyoni ni mama wa huyu na huyu; Mungu Mkuu atauthibitisha.”
6 Mwenyezi-Mungu ataandika katika kitabu, atakapoorodhesha watu: “Huyu amezaliwa huko!”
7 Wote wanacheza ngoma na kuimba: “Siyoni, chanzo chetu ni kwako.”

Generic placeholder image