133

Uzuri wa umoja kati ya watu
(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)
1 Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja.
2 Ni kama mafuta mazuri yatiririkayo kichwani, mpaka kwenye ndevu zake Aroni, mpaka upindoni mwa vazi lake shingoni.
3 Ni kama umande wa mlima Hermoni, uangukao juu ya vilima vya Siyoni! Huko Mwenyezi-Mungu ameahidi kuwabariki watu wake, kuwapa uhai usio na mwisho.

Generic placeholder image