128

Tuzo kwa jamaa imchayo Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake.
2 Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka.
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako.
4 Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu.
5 Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako.
6 Uishi na hata uwaone wajukuu zako! Amani iwe na Israeli!

Generic placeholder image