134

Msifuni Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1 Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.
2 Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu!
3 Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni; yeye aliyeumba mbingu na dunia.

Generic placeholder image