82

Mungu mtawala mkuu
(Zaburi ya Asafu)
1 Mungu anasimamia baraza lake; anatoa hukumu katika kusanyiko la miungu:
2 “Mpaka lini mtaendelea kuhukumu bila haki na kuwapendelea watu waovu?
3 Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara.
4 Waokoeni wanyonge na maskini, waokoeni makuchani mwa wadhalimu.
5 “Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu! Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu! Misingi yote ya haki duniani imetikiswa!
6 Mimi nilisema kuwa nyinyi ni miungu; kwamba nyote ni watoto wa Mungu Mkuu!
7 Hata hivyo, mtakufa kama watu wote; mtaanguka kama mkuu yeyote.”
8 Inuka ee Mungu, uuhukumu ulimwengu; maana mataifa yote ni mali yako.

Generic placeholder image